Habari Mpya
-
24
October
2020RAIS MAGUFULI AZINDUA HUDUMA ZA USAFIRI WA TRENI KATI YA DAR ES SALAAM, TANGA NA ARUSHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli azindua rasmi huduma za usafiri wa treni kati ya Dar es Salaam, Tanga na Arusha, katika Stesheni ya Arusha Oktoba 24, 2020. Soma zaidi
-
16
October
2020WASANII, WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA DAR - RUVU
Wasanii wa tasnia mbalimbali pamoja na waandishi wa habari wamepata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Ruvu mkoani Pwani. Soma zaidi
-
11
October
2020WAZIRI KAMWELWE AZINDUA KICHWA CHA TRENI, VINGINE SITA KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua kichwa kimoja cha treni kati ya vichwa saba vilivyofanyiwa ukarabati katika Karakana ya Morogoro, hafla hiyo imefanyika katika Stesheni ya Dodoma Oktoba 11, 2020. Soma zaidi
-
10
October
2020SHULE YA MSINGI ITIGI RELI YAHAMASISHA SHULE NYINGINE KUTEMBELEA MRADI WA SGR ILI KUJIFUNZA ZAIDI
Walimu na Wahitimu wa Elimu ya Msingi katika Shule ya Itigi Reli watembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Morogoro – Makutupora ambapo mbali na kuona mradi huo wametoa rai kwa shule nyingine kutembelea mradi huo ili kujifunza zaidi, Oktoba 10, 2020. Soma zaidi
-
08
October
2020RAIS WA MALAWI AIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA UJENZI WA RELI YA KISASA – SGR
Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Lazarus Chakwera atembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR kipande cha Dar Es Salaam – Morogoro katika eneo la Ilala jijini Dar es Salaam, ziara hiyo imefanyika tarehe 08 Oktoba, 2020. Soma zaidi
-
05
October
2020MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AONGOZA VIONGOZI WA DINI KUTEMBELEA STESHENI YA SGR
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Abubakar Kunenge akiambatana na viongozi wa Dini wa mkoa wa Dar es Salaam wametembelea jengo la Stesheni ya reli ya kisasa – SGR lililopo Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2020. Soma zaidi