Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Mradi Dar - Moro

Kipande cha kwanza kati ya Dar es salaam na Morogoro kilisainiwa tarehe 3 Februari 2017, ujenzi ulianza tarehe 2 Mei 2017.

Gharama za Mradi

Kwa Kipande cha Dar es Salaam - Morogoro ni Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.7

Ujenzi wa Madaraja

Ujenzi wa daraja refu (Viaduct) la treni ya Umeme kutoka Stesheni ya Dar es Salaam hadi Ilala lenye urefu wa Km 2.56 ili kuepusha msongamano wa waenda kwa miguu, Magari na vyombo vingine vya usairi vinavyotoka na kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Hata hivyo kutakuwa na jumla ya madaraja 26 makubwa na madogo 243 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro. Vivuko vya binaadamu, wanyama na magari vya juu 17 na vya chini 15

Ujenzi wa Stesheni

Jumla ya Stesheni Sita zitajengwa kati ya Dar es salaam na Morogoro, stesheni kubwa mbili ambazo ni za Dar es Salaam na Morogoro, pamoja na stesheni ndogo nne ambazo ni Pugu, Soga, Ruvu na Ngerengere. Usanifu wa Stesheni hizi umezingatia mazingira ya kitanzania, utamaduni na Maliasili zinazopatikana Tanzania vikiwemo vito vya thamani.

Stesheni ya Dar es Salaam ina sura ya madini adimu ya Tanzanite. Stesheni ya Morogoro itaonesha uhasilia wa milima ya Uluguru.

Mfumo wa uendeshaji Treni( Electrifacation Line)

Katika mradi huu treni zitaendeshwa kwa kutumia nishati ya umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania - TANESCO na tayari taratibu za kumpata mkandarasi wa kujenga njia za umeme upo katika hatua za mwisho.

Mfumo wa Mawasiliano (Telecomunication& Signalling)

Mfumo waKisasa zaidi uitwao kwa kitaalamu European Train Control System Level 2 utatumika na kuongeza ufanisi wa uendeshaji na usalama wa treni ambapo treni zitaongozwa kupitia kituo maalum (Central Train Control).

Karakana Kuu na Kituo cha kuunganishia mabehewa.

Kutakuwa na karakana kubwa na Kituo kikuu cha kuunganishia treni zenye urefu wa kilometa mbili kinachojengwa katika eneo la Kwala wilayani Kibaha.