Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Usafirishaji wa Shehena

Tunatoa huduma ya usafirishaji wa mizigo kwa wateja wetu kupitia reli ya Kati na reli ya Tanga ambapo mizigo ya aina tofauti inasafirishwa ndani ya nchi na nchi jirani za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri Demokrasia ya Kongo kupitia Isaka, Mwanza na Kigoma.

Njia Zetu

KUTOKA

  • KWENDA
  • BIDHAA

Dar essalaam

  • Mwanza
  • Mizigo Mchanganyiko

Dar es salaam

  • Kigoma
  • Mizigo Mchanganyiko

Pongwe

  • Mwanza
  • Saruji

Dar es salaam

  • Isaka
  • Mizigo Mchanganyiko

Urambo

  • Morogoro
  • Tumbaku

Dar es salaam

  • Tabora
  • Vida za Mafuta na Mizigo Mchanganyiko

Tabora

  • Dar es Salaam
  • Tumbaku, Mbao na Mifugo

Shinyanga/Bukwimba

  • Dar es Salaam
  • Pamba na Mashudu

Mwanza/Kigoma

  • Dar es Salaam
  • Kahawa na Cinchona Barcks

Tanga

  • Isaka, Kigoma, Mwanza
  • Mizigo Mchanganyiko

Treni ya Mizigo ya Moja kwa Moja

Treni hizi maalum za Mizigo zinawezesha kupunguza muda wa uchelewashaji njia kutokana na kutokuhitaji kukata baadhi ya mabehewa njiani n.k Huduma hii inaweza kuwa ya mteja mmoja kwenda kituo kimoja na wateja zaidi ya mmoja kuelekea kituo kimoja.

Upangaji wa Mabehewa

Tunayo mabehewa ya aina tofauti kwa ajili ya kubebea mizigo ya wateja wetu, mteja atapangiwa behewa kulingana na aina ya bidhaa anayotaka kusafirisha. Kuna mpango maalum unaowawezesha wateja kupangiwa behewa au mabehewa mapema, utaratibu huu unapunguza maombi mengi ya papo kwa hapo yanayosababisha msongamano wa maombi.

AINA YA BEHEWA

  • BIDHAA
">

CCB-Container Carrier Bogie

  • Kubeba Makasha ya Chuma

HLB (C)-High Large Bogie

  • Kubeba Makasha ya Chuma, Mabomba, Mbao, Magogo na Vyuma.

CLB-Covered Large Bogie

  • Kubeba Mizigo aina zote, Sukari, Saruji, Chumvi, Pamba, Tumbaku na Kahawa.

HLB(O)-High large bogie ordinary

  • Kubeba Mabomba, Mbao, Magogo na Vyuma.

BHB-Ballast Hopper Bogie

  • Kubeba Ballast

PTB-Petroleum Tank Bogie

  • Kubeba Mafuta ya Petroli, Mafuta ya Dizeli na Mafuta.

MGB-Motor Goods Bogie

  • Kubeba Magari, na Mizigo ya Jumla(Midogo Midogo).

CWB-Cattle Wagon Bogie

  • Kubeba Mifugo

Kontena

Shirika linalo uwezo wa usafirishaji wa makasha ya kubeba mizigo kwa kutumia mabehewa maalum kama CCBS, LSB(c), HLB(c). Pia kuna Krini maalum aina ya RMG inayotoa huduma ya kupakia na kupakua makasha ya chuma katika mabehewa yetu katika Bandari ya Dar es Salaam, hii inarahisisha upatikanaji wa haraka kontena zinazoendelea na safari.

Ulinzi na Usalama

Kuhakikisha huduma salama za treni na kuepuka ajali, idara ya usalama wa njia inahakikisha kuwa, ukarabati wa njia ya reli, vitendea kazi na mitanbo, ratiba ya mipango ya matengezo ya njia ya reli pamoja na mitambo injini na mabehewa. Ulinzi wa Mizigo ya wateja tokea sehemu ya kupakia hadi kituo cha mwisho inahakikiwa na idara ya ulinzi wa ndani na kikosi maalum cha Polisi Reli kuhakikisha hakuna wizi au upotevu wa mali za wateja katika mabehewa na mali za abiria wanaosafiri na treni zetu.


Kwa Maelezo zaidi

Simu ya Bure; 0800110042

Barua Pepe; trc.care@trc.co.tz