Kuhusu SGR
SRG ni nini?
SRG ni ufupisho wa neno la kiingereza “Standard Gauge Railway”.
Ni reli ya kisasa yenye upana wa mita 1.435, na inayopatikana duniani kote kwa zaidi ya asilimia hamsini na tano (55%).
Tofauti na reli ya kawaida, reli hii inaweza kusafirisha uzito mkubwa na kusafiri kwa mwendo kasi.
TANZANIA NA SGR
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia shirika la reli Tanzania (TRC) imeazimia kujenga reli hii ya kisasa kueneza mtandao usiopungua km 2,561 ikiunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi na nchi zinazokuwa na bandari (Rwanda, Burundi, DRC).
SGR ni reli ya kisasa na ya kwanza Africa mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya umeme na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa.
Lengo la reli hii ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa;
- Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo.
- Uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
- Ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.
- Oboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayo pitiwa na mradi.
- Kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.
- Faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.
Ujenzi wa reli ya kisasa kwa nchi yetu wenye mtandao wa km 1,219 za njia kuu, upo katika awamu tano na ni kama ifuatavyo;
- ØAwamu ya 1 Dae es Salaam – Morogoro (Km 300)
- ØAwamu ta 2 Morogoro- Makutupora (Km 422)
- ØAwam ya 3 Makutupora –Tabora (Km 294)
- ØAwamu ya 4 Tabora – Isaka (Km 130)
- ØAwaam ya 5 Isaka – Mwanza ( Km 249)
Awamu ya kwanza: Dar es salaam – Morogoro (Km 300). Ujenzi wa reli ya kisasa kwa awamu ya kwanza ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano. Dr John Pombe Magufuli siku ya tarehe 12, april 2017. Na kwa sasa ujenzi bado unaendelea chini ya mkandarasi YAPI MERKEZI kutoka Uturuki akishirikiana MOTA ENGIL AFRICA kutoka Ureno.
Awamu ya pili: Morogoro - Makutupora ( Km 442). Ujenzi wa mradi ulizinduliwa na Rais wa awamu ya tano. Dr John Pombe Magufuli siku ya tarehe 14, machi 2018. Na kwa sasa hatua za awali za ujenzi zimeanza chini ya mkandarasi YAPI MERKAZI.
Awamu ya 3, 4, na 5: Awamu hizi, ziko katika hatua mbalimbali za manunuzi.
MUUNDO NA MPANGILIO WA RELI YA KISASA (SGR)
Reli hii ya kisasa inajengwa sambamba na reli iliyopo (MGR) isipokuwa maeneo maeneo machache yenye kona kali. Ujenzi wa reli hii unazingatia uhifadhi wa mazingira na usalama wa watu na mali zao.
- Sehemu za mwingiliano wa magali na reli, kutakuwa na aidha kivuko cha juu na chini.
- Uzio unajengwa kwa usalama wa watu na wanyama.
- Elimu kuhusiana na usalama kwa ujumla itatolewa mara kwa mara.
UTWAAJI WA ARDHI NA ULIPAJI FIDIA KWA WAATHIRIKA WA MRADI WA SGR
Kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1999na sheria ya tathmini ya mwaka 2016, maeneo yote yanayo pitiwa na mradi ambayo hayamilikiwi na shirika la reli Tanzania (TRC) yatafanyiwa tathmini, kutwaliwa na wamiliki wa maeneo hayo watalipwa.