Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Usafiri wa Abiria

Kwanini Usafiri na Shirika la Reli Tanzania?

kusafiri na reli ni zaidi ya safari, maana utapata fursa ya kuona mandhari nzuri ya nchi ya Tanzania, uoto wa asilimbuga za wanyama, huduma bora za chakula katika mgahawa ndani ya treni pamoja na huduma za afya.Usafiriumepangiliwa kwa kuzingatia ratiba zilizowekwa kwa mpangilio ukilinganishana aina nyingine za usafiri.

1. Usalama kwanza

Usalama ni kitu cha kwanza katika safari za TRC, Shirika linafuata taratibu za kiutendaji ili kuhakikisha usalama kwa wateja na afya za abiria na wahudumu wa treni kwa kuhakikisha hilo ndani ya treni za TRC kuna behewa kwa ajili ya huduma za afya vipo vifaa muhimu kwa ajili ya usalama ikiwemo sanduku la huduma ya kwanza vifaa vya kuzimia moto. Shirika lina wahudumu waliofuzu kitaaluma kwa viwango vinavyohitajika.Treni ili kuhakikisha usalama wa abiria .Shirika linatumia mfumo wa kisasa kutambua mienendo ya treni zinapokuwa kwenye safari.

2. Usafiri wa Gharama nafuu Nafuu

Usafiri wa TRC ni nafuu zaidi ukilinganisha na aina nyingine za usafiri kutokana na kuwepo kwa madaraja tofautii ambayo yanatoa fursa kwa watu wa vipato vya aina zote kusafiri.

3. Mwendokasi kwa umbali mrefu

Kutokana na kutokuwepo kwa vikwazo vinavyoweza kufanya safari kuwa ya muda mrefu kwa sababu ya msongamano, kasi ya usafiri wa TRC imekuwa ile ile tangu mwanzo hadi mwisho wa safari kwa umbali mrefu zaidi.

4. Nafasi ya kuona na kutalii

Unapokuwa kwenye mabehewa ya abiria unapata nafasi ya kuhama kutoka behewa moja kwenda behewa linginena kufurahia muonekano mzuri wa maeneo asilia na vivutio mbalimbali.

Treni

Treni ya Deluxe

Hii ni treni ya kisasa ya abiria ambayo inafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Tabora, Mpanda na Kigoma pembezoni mwa ziwa Tanganyika.

Huduma ya Chakula; Uwapo kwenye treni ya Deluxe utafurahia hduuma nzuri ya chakula kilichoandaliwa na wapishi hodari pamoja na vinywaji mbali mbali. Tuna wapishi na wahudumu hodari watakaokuhudumia pindi uwapo kwenye behewa maalum la Chakula lililosheheni vyakula mbali mbali na kukufanya ufurahie safari yako.

Simu na Mtandao; Ili kukufanya abiria ujisikie uko safarini matumizi ya Simu na vifaa vingine vya mawasiliano vimewekewa mazingira mazuri ya kukufanya uweze kupata huduma za mawasiliano muda wote uwapo safarini.

Mabehewa yenye nafasi ya kutosha yanakupa nafasi ya kutembea kutoka behewa moja hadi lingine na kufurahia muonekano mzuri wa maeneo asilia na vivutio mbali mbali. Treni ya Deluxe inayo mabehewa ya Daraja la Pili Kulala, Daraja la Pili Kukaa pamoja na Daraja la Tatu.

Treni ya Ordinary

Treni mbili za Ordinary zinafanya Safari zake mara mbili kwa wiki kutoka Dar es Salaam, Tabora hadi mwanza. Treni ya Ordinary ina Mabehewa ya Daraja la Kwanza Kulala, Daraja la Pili Kulala, Daraja la Pili Kukaa na Daraja la Tatu ikiwa na behewa maalum la Mgahawa kwa ajili ya Chakula na Vinywaji.

Treni ya Mjini

Shirika la Reli Tanzania(TRC) linatoa huduma ya usafiri wa treni za mjini ambazo zinafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Pugu kupitia Kamata, Bungoni, Bakhresa, Vingunguti, Kipawa, Airport, Banana, Mombasa na Gongo la Mboto umbali wa km 20 pamoja na Dar es Salaam-Ubungo kupitia Kamata, Bakhresa, Buguruni kwa Mnyamani, Tabata Matumbi, Tabata Mwananchi/Relini na Mabibo umbali wa km 12. Huduma ya Treni za mjini inapatikana Asubuhi na Jioni siku za Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamis na Ijumaa. Nauli za treni za mjini ni Shilingi 600 kutoka Dar es Salaam hadi Pugu kwa mtu mzima, Shilingi 400 kutoka Dar es Salaam hadi Ubungo kwa mtu mzima na Shilingi 100 kwa Mwanafunzi.


Kwa maelezo zaidi

Simu ya Bure; 0800110042

Barua Pepe; trccare@trc.co.tz