Moro-Makutupora Project
Mpango kazi mradi wa SGR kutoka Morogoro hadi Makutupora (Manyoni) unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2021. Kipande cha Morogoro Makutupora chenye kilomita 422 kinajengwa na Kampuni ya YAPI MERKEZI ambacho mkataba wake umesainiwa Sepemba 29, 2017.
Gharama za Mradi
Kipande cha Morogoro Makutupora ni kiasi cha shilingi za Kitanzania Trilioni 4.4
Maendeleo ya Ujenzi
Mkandarasi yupo kwenye hatua ya Kusafisha eneo la Ujenzi pamoja na ujenzi wa tuta.
Mfumo wa uendeshaji Treni(Electrifacation Line)
Katika mradi huu treni zitaendeshwa kwa kutumia nishati ya umeme kutoka Tanesco na tayari taratibu za kumpata mkandarasi wa kujenga njia za umeme upo katika hatua za mwisho.
Mfumo wa Mawasiliano na Ishara (Telecomunication& Signalling)
Mfumo waKisasa zaidi uitwao kwa kitaalamu European Train Control System Level 2 utatumika na kuongeza ufanisi wa uendeshaji na usalama wa treni ambapo treni zitaongozwa kupitia kituo maalum (Central Train Control).