Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Tabora - Isaka Project

Mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Tabora – Isaka umesainiwa kati ya TRC na kampuni ya Yapi Merkezi kutoka nchini Uturuki ikiwa ni ukamilishaji wa sehemu ya ujenzi wa reli ya kisasa awamu ya kwanza Dar es Salaam – Mwanza yenye vipande vitano.

Kipande cha Tabora hadi Isaka kina jumla ya kilomita 165 ambapo kilomita 130 ni njia kuu na kilomita 35 ni njia za kupishania. Thamani ya mkataba wa ujenzi ni Dola za kimarekani milioni 900.1 sawa na fedha za kitanzania trilioni 2.094, muda wa utekelezaji ni miezi 42 ikijumlisha muda wa majaribio wa miezi 6

Kipande hiki kitakuwa na jumla ya Stesheni 3 ambazo ni Nzubuka, Ipala Bukene pamoja na Karakana Kuu itakayojengwa Tabora