Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara



Nawezaje kukata tikiti yangu?

Unaweza kukata tikiti yako kwenye kituo cha treni kilicho karibu nawe na kuchagua aina ya daraja unalopendelea. Unahitaji kuwa na kitambulisho kitakachokuwezesha kukata tikiti. Vitambulisho vinavyotumika ni, Cha kupigia kura, Cha uraia, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha kazi, Kadi ya bima ya afya, na barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa. Pia treni zetu zote za abiria unaweza kukata kabla tikiti za daraja la Kwanza na Pili, na daraja la tatu kama kuna sababu maalum ya kufanya hivyo.

Je, Nahitaji kitambulisho ninaposfiri na treni?

Ndiyo, Unahitaji kuwa na kitambulisho wakati wa kusafiri kwa sababu za kiusalama pia kutambua abiria. Vitambulisho vinavyohitajika ni pamoja na kadi ya kupigia kura, leseni ya udereva, kitambulisho cha utaifa, kitambulisho cha kazi, kadi ya bima ya afya na barua ya serikali ya mtaa.

Jinsi ya kuahirisha safari

Unaruhusiwa kubadili siku ya safari iwapo utatutaarifu masaa matatu kabla ya treni kuanza safari, na endapo siku utakayochagua kusafiri itakuwa na nafasi unayoomba.

Naweza kurudishiwa gharama za tikiti, baada ya kukata, na nifanyeje?

Ndio, unaweza kulipwa rejesho la gharama za kukata tikiti zilizokatwa iwapo mteja atatutaarifu masaa matatu kabla ya treni kuanza safari zake, abiria akishindwa kufanya hivyo marejesho ya gharama ya tiketi hayatafanyika, unapotoa taarifu mapema unatusaidia kumpa mtu mwingine nafasi ya kusafiri.
kwa sababu zingine abiria anaweza akafungua madai kwa hatua zifuatzao;
1. Taarifa ya kupotea
2. Fomu ya madai kutoka kwa mdaiwa
3. Fomu ya mteja ya madai
4. Risiti halisi ya madai
5. 5 .Ripoti ya ajali
6. Simu ya maandishi
7. Kipande cha karatasi


Je, mnatoa huduma ya Vinywaji Chakula?

Ndio, tunatoa huduma ya Chakula na Vinywaji kwa gharama zako.

Je, Ni salama kusafiri na Treni?

Usalama ni kitu cha mwanzo kabisa katika safari zetu, tunafuata taratibu za kiutendaji ili kuhakikisha usalama na afya ya abiria na wahudumu wetu wa treni. Tunao wahudumu waliofuzu kitaaluma kwa viwango vinavyohitajika pia tunaendesha mafunzo na semina za mara kwa mara kutathmini utendaji wa wahudumu wetu kwenye treni zetu.
Ili kuhakikisha usalama wa abiria na wahudumu wetu tunavyo vifaa muhimu kwa ajili ya usalama ikiwemo sanduku la huduma ya kwanza, vifaa vya kuzimia moto n.k. Pia tunatumia mfumo wa kisasa kutambua mienendo ya treni zinapokuwa kwenye safari.

Kuna tofauti gani kati ya MGR NA SGR?

.Mita geji ni aina ya njia ya treni ambayo ina upana wa mita 1yenye uwezo wa kutembea usiozidi kilometre kwa saa,na uwezo wa kubeba mizigo isiyozidi tani 5,000,000 kwa mwaka.reli ya kisasa ni aina ya reli yenye upana wa mita 1435 au 1.345 na inauwezo wa kutembea spidi 160 kwa saa na kubeba mizigo ya usiyozidi tani 25,000,000

Je, Mnatoa huduma ya

...

Je Mnasafirisha Mizigo?

.

...

..