Bandari Kavu
Bandari Kavu-Isaka
Kituo hiki cha Kontena kimesajiliwa kama Bandari kavu mwezi Septemba Mwaka 1999. Hii inamaanisha Bandari ya Dar es Salaam sasa inasogea karibu zaidi na nchi za Rwanda, Burundi, DRC(Congo) na Uganda. Kinachotakiwa ni kuweka anwani inakoelekea Mzigo(“Through Bill of lading au Combine Transpor Document”) kwa Mizigo itakayoelekezwa Banadari hiyo ya Isaka.
Uwezo wa Kuhudumia Shehena
- Bandari hii ina ukubwa wa Hekta 11,04
- Bandari hii ina uwezo wa kuhudumia 13,000 TEUS katika eneo lake la Mita za Mraba 12,350 m2
- Inaweza kuhudumia 42,583 MT kwa mwaka
- Zipo Ghala mbili za Mizigo midogo midogo inayoendelea na Safari.
- Katika Bandari ya Isaka kuna Mawasiliano ya Simu, Nukushi na Mfumo Maalum wa Kusimamia shehena(Advanced Cargo Information System)
- Kuna Ghala mbili zenye uwezo wa kuhifadhi mzigo wa Tani 7,000.
- Kuna Ghala la Mafuta lenye uwezo wa kuhifadhi lita 2,000,000 za bidhaa ya Mafuta.
- Uwezo wa kuhifadhi Vida hadi 240,000MT ya mizigo midogo midogo iliyo kwenye gunia.
- Eneo lingine chini ya (Hadas) linao uwezo wa kuhifadhi Lita 1,600,000 za vida ya mafuta.
- Kuna njia mbili za reli zenye uwezo wa kuhudumia behewa 11 kwa wakati mmoja
- Kuna mitambo maalumu ya kubebea mizigo, mmoja wenye uwezo wa kubeba Tani 6, wenye uwezo wa kubeba Tani 5 na miwili yenye uwezo wa kubeba Tani 3 kila moja.
- Kuna Krini yenye uwezo wa Tani 32
- Pia kuna Krini ya kupangia Kontena ya futi 20 na futi 40.
- Kuna Jenereta lenye uwezo wa 27KVD.