Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Makutupora - Tabora Project

Ujenzi wa Reli ya Kisasa Makutupora – Tabora unahusisha ujenzi wa reli yenye urefu wa jumla ya kilomita 368 ambapo kilomita 294 ni njia kuu na kilomita 74 ni njia za kupishania, ambapo hamani ya mkataba wa ujenzi ni Dola za Marekani bilioni 1.908 sawa na Shilingi trilioni 4.406, muda wa ujenzi ni miezi 46 ikijumlisha muda wa majaribio.

Kipande cha SGR Makutupora – Tabora kitakuwa na vituo vya abiria na mizigo vipatavyo nane (8) ambavyo ni Manyoni, Itigi, Kazikazi, Tura, Malongwe, Goweko, Igalula na Tabora, pamoja na kituo cha uendeshaji treni cha dharura Tabora, hii ni endapo ikitokea hitilafu katika kituo kikuu (OCC) Dar es Salaam treni ziweze kuongozewa kutokea tabora bila kusimamisha kazi za uendeshaji.