Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

Disclaimer

Taarifa zilizomo kwenye tovuti hii ni kwa ajili ya matumizi ya Shirika la Reli Tanzania. Taarifa hizi zinatolewa na Shirika la Reli Tanzania na nakuna madai yatakayotolewa kuhusu usahihi, ukamilifu, upatikanaji, uaminifu au uhalali wa maudhui (taarifa, picha, huduma, bidhaa) ya tovuti hii kwa lengo lolote.

Taarifa zilizopo kwenye tovuti ya Shirika la Reli Tanzania zinatolewa kwa kuzingatia kwamba wanaotembelea tovuti hii wanalo jukumu la kuchambua taarifa zilizo kwenye tovuti hii ili kuhakiki usahihi wa taarifa hizo, Shirika la Reli halitahusika na yeyote atakayetumia vibaya taarifa zilizomo kwenye tovuti hii.

Tovuti ya Shirika la Reli Tanzania inaweza kuwaunganisha na wavuti za tovuti za nje zilizo za serikali au zisizo za serikali (Tovuti za mtumiaji wa tatu) isipokuwa pale itakapoelekezwa, vinginevyo Shirika la Reli Tanzania halitahusika na usahihi wa taarifa zilizopo kwenye mitandao hiyo wala kushirikiana kwa vyovyote na wanaondesha mitandao hiyo.

Jitihada za kuhakikisha tovuti inakuwa hewani muda wote zinafanyika. Japokuwa Shirika la Reli Tanzania halitawajibika na tovuti kutokuwa hewani kutokana na sababu za kiufundi zilizo nje ya uwezo wetu.

Kama una maswali yoyote yanayohusiana na maudhui ya tovuti yetu ,

Tafadhali Wasiliana nasi

Barua pepe; info@trc.co.tz

Tovuti; www.trc.co.tz