Privacy Policy
Taarifa binafsi zinazokusanywa na Shirika la Reli Tanzania zitatumiwa na Shirika la Reli Tanzania tu. Tutatumia taarifa zako kujibu maswali, maoni au malalamiko kulingana na matakwa yako. Hatutatoa taarifa zako sehemu nyingine yoyote(mtu wa tatu) nje ya Shirika la Reli Tanzania.
Shirika la Reli Tanzania linaweza kukusanya taarifa zako kupitia mtandao unapotembelea tovuti yetu. Taarifa zinazoweza kukusanywa ni pamoja na;
- Kurasa unazotembelea
- Anuani ya mtandao unazotumia kutembelea tovuti
- Tarehe na muda uliotembelea tovuti
- Aina ya njia uliyotumia kutembelea tovuti yetu
- Taarifa zako unazojaza unapotutumia maoni au maswali
- Shughuli ulizofanya ambazo zimefanikiwa na ambazo hazijafanikiwa
Shirika la Reli Tanzania linatumia taarifa zako zinazokusanywa na mtandao wetu kwa lengo la kuboresha huduma zetu, kwa kupokea maswali, maoni na malalamiko kwa lengo la kuyafanyia kazi kwa manufaa ya watumiaji tu.
Tunachukua tahadhari kulinda taarifa zako muhimu unapotutumia kupitia tovuti yetu, taarifa zako zitalindwa muda wote. Kwa ajili ya usalama wa tovuti yetu na kuhakikisha tovuti yetu inakuwa hewani kwa watumiaji, Shirika la Reli Tanzania limeajiri wataalamu ambao wanasimamia shughuli za mtandaoni kwenye tovuti yetu ili kujua majaribio ambayo yanaweza kusababisha upotoshaji wa taarifa zetu.