Habari Mpya
-
21
May
2018SHIRIKA LA RELI TANZANIA LASAINI RASMI MKATABA WA UNUNUZI WA INJINI MPYA 11 ZA TRENI
TRC yasaini mkataba na Kampuni ya Progress Rail Locomotives (PRL) ya Marekani inayomiliki vichwa vya treni 11 vilivyoletwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuvinunua vichwa vyenye namba 9014, 9015, 9016, 9017, 9018, 9019, 9020, 9021, 9022, 9023 na 9024. Soma zaidi
-
09
May
2018WAZIRI MBARAWA ATANGAZA RASMI SHERIA MPYA YA RELI TANZANIA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa ametangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria mpya ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017. Katika tukio hilo lililofanyika mbele ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Prof. John Wajanga Kondoro. Soma zaidi
-
09
May
2018WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATEMBELEA KUONA UJENZI WA RELI KISASA
Waziri Prof. Mbarawa atembelea ujenzi wa reli ya kisasa na kukagua ujenzi wa tuta na kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege na kumtaka mkandarasi Yapi Markes na Motaengel Africa anayejenga reli hiyo kutoka Dar es Sakaam hadi Morogoro kilomita 205 kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya wakati. Soma zaidi
-
09
May
2018MKATABA WA UJENZI WA RELI YA KISASA AWAMU YA PILI KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA WASAINIWA
Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli imeingia mkataba na Kampuni ya Yapi Merkezi kujenga kipande cha pili cha reli ya kisasa(SGR) kutoka Morogoro hadi Makutopora yenye urefu wa kilomita 336 za njia kuu na kilomita 86 za njia za kupishana treni na maeneo ya kupangia mabehewa jumla kilomita 422.. Soma zaidi