Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC LAENDELEA NA ZOEZI LA KUHAMISHA MAKABURI KIPANDE CHA MOROGORO- MAKUTUPORA


news title here
23
September
2019

Shirika la Reli Tanzania liko katika Zoezi la kuhamisha makaburi kwa kushirikiana na wananchi ambao wanahusika na makaburi hayo katika maeneo ambayo ujenzi wa Reli ya Kisasa utapita katika vijiji na vitongoji vilivyopo Dodoma na Singida.



Lengo la zoezi la uhamishaji makaburi ni kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongogozwa na Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli katika maamuzi ya kuwezesha na kuboresha miundombinu ya reli hasa ujenzi wa reli ya kisasa.



Makaburi yatakayopitiwa na ujenzi wa reli ya kisasa ni 34 na mpaka sasa yameshahamishwa na kupelekwa sehemu maalumu iliyopo Makutopora ambayo imepangwa kuhifadhi miili ya marehemu.



Katika zoezi hili la uhamishaji wa makaburi Shirika la Reli Tanzania linashirikiana na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya, Halmashauri, wenyeviti wa vijiji, madiwani,Watendaji Kata ,Vitongoji pamoja na mafisa ustawi wa jamii na wilaya.



Wakati zoezi la kuhamisha makaburi linaendelea Shirika la Reli Tanzania-TRC linawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kila mwananchi ambae eneo lake limepitiwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa-SGR watalipwa fidia