SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC KUBEBA MAONO YA MAENDELEO YA UCHUMI WA NCHI ZA SADC:
September
2019
Banda la Shirika la Reli Tanzania -TRC limepata bahati kutembelea na mgenirasmi Mhe.. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa Kassim wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wa nchi16 za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Africa – SADC, Mkutano huo umefanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere – JNICC Septemba 19, 2019 jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulianza septemba 16, 2019 ambapo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alifungua rasmi mkutano kwa kuanza na makatibu wakuu wa Wizara zilizoshiriki kipindi hiki na wakiwa nq wajumbe wengine ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa na soko la pamoja katika sekta ya miundombinu ya uchukuzimawasiliano ifikapo mwaka elfu mbili na hamsini (2050) sekta hizo ambazo ni mhimili mkubwa katika kufikia azma ya maendeleo katika jumuia hiyo iliodumu kwa zaidi ya miongo miwili na nusu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliawa Kassim alifika katika banda la Shirika la reli Tanzania - TRC na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu masanja Kungu Kadogosa na kupewa maelezo kuhusu maendeleo ya miradi mikubwa ya kitaifa inayosimamiwa na Shirika la Reli ikiwemo ujezi wa reli ya kisasa - SGR na uboreshaji wa reli ya kati – TIRP,pamoja na miradi mingine kama ufufuaji wa njia reli Dar es -Salaam -Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu alisisitizaendapo miundo mbinu ya reli ikihimarishwa itasaidia kukuza uhusiano kwa kutoa fursa za kibiasharandani ya jumuia za Nchi za SADC .
Aidha, katika mkutano huo Waziri Mkuu amebainisha mchango wa ujenzi wa reli ya kisasa sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya reli katika kuleta maendeleo ya uchumi kwa wanachama wa jumuiya ya SADC. “kati ya miradi mikubwa inayotekelezwa hapa Tanzania ni ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi inayojengwa katika ukanda wa kati pamoja na ukanda wa reli ya TAZARA ambayo inaunganisha nchi za wanachama wa SADC, reli hizi zitaboresha biashara kati ya Tanzania na nchi za wanachama wa SADC” Waziri Mkuu alisema.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya mawaziri wa wizara hizo, amezungumzia juu ya mpango wa jumiya hiyo katika kuleta maendeleo katika nchi hizo ikiwemo sekta ya uchukuzi kwa njia ya reli “ wajumbe wameleta hoja mbalimbali zikiwemo namna za kushugulikia ujenzi wa miundombinu kama vile Reli, kukabiliana na majanga pamoja na hali ya hewa manufaa ya teknologia ya habari na mawasilianokatika kuboresha uchumi na Maisha ya wana SADC, wataalam kutoka sekta za kibanki wameeleza uwezo wao katika kusaidia ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu katika SADC”alisemaWaziriKamwele.