Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC KINARA UTOAJI ELIMU NA HUDUMA BORA KILELE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


news title here
23
June
2025

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aikabidhi Shirika la Reli Tanzania (TRC) cheti maalum cha Utambuzi wa utoaji Elimu na Huduma bora katika jamii kwenye hafla ya kilele cha wiki ya utumishi kwa umma iliofanyika viwanja vya Chinangali park jijini Dodoma Juni 23, 2025.

Mhe. Kassim majaliwa ameipongeza TRC na Taasisi nyingine za umma kwa kubuni na kuendelea kutumia mifumo ya kidigit yenye ufanisi kuhudumia jamiii.

"Mifumo hii ya kidigiti imeleta mabadiliko katika utumishi wa umma, imeongeza uharaka, ufanisi, kuzuia rushwa na urasimu katika kutoa huduma, hii ni hatua nzuri sana yakupongezwa" Amesema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Mhe. Majaliwa amezitaka Taasisi zote za umma kujiunga na mifumo ya kidigit ambayo itawawezesha kusimana na kurahisisha utekelezaji majukumu na kutoa huduma kwa haraka kwenye jamii.

Naye Mkurugenzi Idara ya Rasilimali watu na Utawala kutoka Shirika la Reli Tanzania Bi. Irene Ungani- Kyara ametoa wito kwa wafanyakazi wote wa TRC kuendelea kufanya kazi kwa nidhamu, weledi na utayari katika utoaji huduma.

"Nichukue fursa hii kuwapongeza washiriki wote katika maonesho haya ya wiki ya utumishi kwa ushindi, lakini pia nawapongeza wafanyakazi wote wa TRC kwa kazi nzuri wanayofanya, nipende kusema TRC itazidi kuboresha huduma na kuwasaidia watanzania wote" Amesema Bi.Irene.

Katika kuendelea kukuza uchumi wa nchi na kuonesha uzalendo watumishi wametakiwa kufanya kazi wa uzalendo na kufuata kanuni na miongozi ya yakiutumishi.