Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC KUSHIRIKIANA NA TMA KUJENGA MIUNDOMBINU YA RELI YENYE UBORA NA IMARA.


news title here
03
August
2025

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imeahidi kuendelea kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania ( TRC ), kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya reli inajengwa kwa uimara na ubora kwa kuzingatia hali ya hewa ya kijografia ya kila eneo linalopitiwa na Reli.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Ladislaus Chang'a alipolitembelea banda la TRC katika maonesho ya Nane Nane yaliyoanza viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma, Agosti Mosi na kutarajiwa kufikia tamati yake Agosti 8, 2025.

Kwa upande mwingine Dk. Ladislaus amesema TRC iendelee kuboresha mifumo ya kidigiti ya ukataji tikiti wa treni za SGR ili kukidhi mahitaji na kuendana na ongezeko la abiria wanaotumia usafiri wa reli.

"Tangia treni za SGR zimeanza ninetoa waraka kwa Wafanyakazi wote wanapoenda kikazi Dar Es Salaam - Morogoro - Dodoma watumie treni ya SGR kwa kuwa ni salama, bei nafuu na kuchangia pato la Taifa, TRC jitaidini kuboresha mifumo ya kidigiti ya ukataji tiketi kurahisisha huduma" amesema Dk.Ladislaus.

Katika maonesho ya Nanenane 2025 TRC inaendelea kuelimisha umma kuhusu huduma zitolewazo sambamba na fursa za uwekezaji zinazopatikana kupitia uwekazaji mkubwa wa ujenzi wa reli ya SGR ikilenga kukuza sekta ya kilimo, viwanda, Utalii na ajira kwa Watanzania.