Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

UJENZI WA SGR KUZIUNGANISHA TANZANIA NA BURUNDI


news title here
18
August
2025

Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, kwa pamoja wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa SGR kipande cha Uvinza - Musongati katika hafla iliofanyika Msongati Mkoa wa Rutana nchini Burundi Agosti 16, 2025

Ujenzi wa reli ya SGR Kipande cha Uvinza - Msongati unalengo la kuziunganisha Tanzania na Burundi katika nyanja ya kisiasa na kiuchumi huku ikichochea kukua kwa sekta ya usafiri na usafirishaji kwa njia ya reli na bandari ya Dar Es Salaam.

Akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe hilo la msingi Rais wa Burundi Mhe. Ndayashimiye, amesema kuwa anaamini katika umoja uliopo baina ya nchi ya Tanzania na Burundi na kupitia ujenzi wa SGR uhusiano utaongezeka mara dufu.

"Leo ni siku ya Kihistoria nchini Burundi, nyuso za Wanaburundi zimejawa na furaha na watu wanafurahia maendeleo haya, Burundi kwasasa imeamua kupiga hatua kwa kuendeleza sekta za uchukuzi zitakazo chochea maendeleo na kukuza uchumi" amesema Mhe. Ndayishimiye.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na ile ya Burundi kwa kwa kuweka misingi Imara wa Kimkakati kwa kuamua kujenga Reli ya SGR ambayo itasaidia Uchumi wa nchi zote mbili.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa mradi wa ujenzi wa SGR Uvinza - Msongati wenye urefu wa kilomita za mraba 300 ambapo kati ya hizo kilomita 240 ni za njia kuu na 60 ni njia za kupishana utachukua miezi 72 kukamilika na utazalisha takribani tajira 5,000 za moja kwa moja kutoka kwa mkandarasi.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa SGR kipande cha Uvinza - Msongati kutapunguza gharama za usafirishaji mizigo kutoka Bandari ya Dar Es Salaam - Burundi kutoka dola 3800 kwa kasha moja lenye futi 20 mpaka dola 2000 pindi mradi utakapokamilika pia itasaidia SGR itabeba Mizigo mingi kwa wakati mmoja kutoka tani 30( Lori moja) kwasasa hadi tani 3800 kwa mkupuo.

Ujenzi wa reli ya SGR unasisitiza agenda ya nchi za Afrika kujenga miundombinu bora na Imara kuziunganisha nchi za Afrika.