Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA LAKAMILIKA WILAYANI MPWAPWA ILI KUPISHA UJENZI WA RELI YA KISASA


news title here
19
February
2020

Shirika la Reli Tanzania – TRC limekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha pili kutoka Morogoro, Dodoma hadi Makutupora hivi karibuni Februari, 2020.

Maeneo mbalimbali ya Mpwapwa wananchi wamepatiwa hundi zao na asilimia kubwa ya wananchi hao wamekwishahamisha makazi yao na wengine wanaendelea na zoezi hilo la kuhamisha mali na makazi ili kupisha mradi.

Wananchi wameupokea vema mradi huo wa kisasa unaondelea na kufurahishwa kwa kiasi kikubwa kwani imani yao ni mradi kuwaletea maendeleo mbalimbali ikiwemo ya usafiri pamoja na mzunguko wa biashara .

Maeneo ambayo baadhi ya wananchi wanatakiwa kupisha mradi wa SGR wilayani Mpwapwa ni pamoja na kijiji cha Msagali, Mnase, Msamalo, Godegode, Igandu, Chimwaga, Kimagai, Kisisi na Gulwe.

Pia wananchi wamekua wakishiriki vyema katika zoezi hilo na kuwa na imani ya kwamba kupisha mradi huo kutawaletea manufaa katika maeneo yao yaliyopitiwa na reli ya kisasa kwa kuleta chachu ya maendeleo pamoja na ongezeko la ajira kwa vijana.

Zoezi hilo ambalo linaendeshwa na maafisa kutoka Shirika la Reli nchini wakishirikiana na watendaji na wenyeviti wa vijiji wa maeneo hayo ambapo viongozi wa maeneo husika wameipongeza Serikali ya awamu ya tano Shirika la Reli pamoja kwa kuwa na juhudi za kijenga mbiundombinu nchini hususani reli mpya ya kisasa na kutimiza lengo la ulipaji wa fidia kwa wakati.

Mmoja wa Wahasibu wa TRC Bi. Teresia Bwire amesema kuwa changamoto ni nyingi zilijitokeza katika utoaji wa hundi ila ni jambo la kushukuru hadi sasa zoezi limekamilika na wananchi wamekua na uelewa mkubwa wa kupisha mradi kwa haraka ili ujenzi uweze kuendelea.

“Wananchi wengi wameshahamisha makazi yao pamoja na wale wenye maeneo kama mashamba, madampo, na makaburi wameshayaachia, kiukweli wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu” alisema Bi. Teresia Bwire.

Naye Mtendaji kutoka kijiji cha Igandu John Mandela amewakilisha watendaji wa Wilaya ya Mpwapwa kwa kuishukuru sana Serikali ya awamu ya tano ikishirikiana na TRC kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa SGR kwani ni mradi mkubwa sana ambao utaleta chachu ya maendeleo kwa wananchi katika maeneo yote ya nchi.