Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC YAKABIDHIWA ENEO LA ISAKA KWAAJILI YA KUPOKEA MIZIGO KUTOKA BANDARI YA DSM KWENDA NJE YA NCHI


news title here
07
March
2026

Shirika la Reli Tanzania (TRC), limekabidhiwa eneo la Isaka, Mkoani Shinyanga, kwaajili ya kupokea na kushushia mizigo kutoka Bandari ya Dsm na kisha kusafirishwa ndani na nje ya nchi.

Eneo hilo lenye jumla ya mita za mraba 29,450 sawa na ekari 7, lililoko , Isaka Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga lilikuwa linatumika na Shirika la Mpango wa Chakula duniani (WFP) kwaajili ya kusambaza chakula kwenye kambi za wakimbizi katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DR na Sudani Kusini.

Hatua hiyo inalenga kupunguza msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi wa ubebaji wa mizigo na kuisambaza ndani na nje ya nchi.

Makabidhiano ya eneo hilo yamefanyika Machi 7, 2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ambapo Mkuu wa Mkoa huo, Mboni Mhita, akizungumza kwenye makabidhiano hayo amesema wanafarijika TRC, kwa kuamua kulitumia enep kwa ajili ya usafirishaji wa mizigo, sababu Mkoa huo una kongani ya viwanda na kwamba utasaidia wawekezaji kusafirisha mizigo yao kwa wakati na kurahisha ufanyaji wa biashara.

Aidha mkuu huyo wa Mkoa, ameelezea uwekezaji huo wa TRC, pamoja na mambo mengine, unakwenda kuufungua zaidi mji mdogo wa Isaka na maeneo mengine ndani ya Mkoa huo kwa kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, kufungua mianya mingi ya ya mzunguko fedha na uwekezaji mwingine utaotokana na uwekezaji wa TRC kana nyumba za wageni, ambapo serikali pia itapata mapato kutokana na uwekezaji huo.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TRC Bwana Jaffer Machano, alisema, TRC haitaishia kwenye uwekezaji tu pekee bali itakuwa ni wanajamii wema kwa jamii inayozunguka uwekezaji wake mahali hapo.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Machibya Shiwa, alisema kwa upande wa TRC, eneo la Isaka ni moja ya maeneo ya kimkakati, kwamba reli zote mbili zinapoanzia bandari ya Dar es salaam, ni lazima iwe na sehemu ya kushusha mizigo, na eneo hilo ni muhimu sababu nir ahisi kwa usafirishaji wa mizigo kuelekea nchi jirani.

Amesema kwamba, eneo hilo la WFP palijengwa miundombinu ya reli kwa ajili ya kuchukua mizigo na kuipeleka kwenye maeneo ambayo yalikuwa yameathirika na vita kama Rwanda, Burundi, DRC na Sudani Kusini.

Amesema, eneo hilo la WFP litatumika kuipungumzia mizigo Bandari ya Dar es salaam,na kuileta Isaka kupitia Reli ya MGR ili kuongeza ufanisi wa ubebaji wa mizigo.

“Hiki tunachokifanya Mkuu wa Mkoa ni mkakati wa muda mfupi, ni kuisaidia Bandari ya Dar es salaam kuchukua mzigo kuleta Isaka, sababu sasa hivi kuingia Bandari ya Dar es salaam kunachangamoto kubwa,” amesema Mhandisi Shiwa.

Ameongeza kuwa katika mkakati wa muda mrefu, TRC inapanga kujenga kituo cha reli ya kisasa ya SGR katika eneo la Isaka kwa ajili ya kuiongezea uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam, na kwamba wafanyabiashara wengine watakuwa wakiagiza mizigo yao moja kwa moja katika Bandari Kavu ya Isaka badala ya Dar es Salaam.