Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​ZOEZI LA KUHAMISHA MAKABURI KUONGEZA KASI YA MRADI WA SGR MORO -MAKUTUPORA


news title here
13
June
2019

Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na zoezi la kuhamisha makaburi katika maeneo ambayo Reli ya Kisasa - SGR inapita kuanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, hivi karibuni Juni 2019.

Zoezi linaendelea kwa lengo la kumkabidhi maeneo Mkandarasi ili aweze kuendelea na kazi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Morogoro -Makutupora Singida ambao umefika zaidi ya 10%.

Aidha awamu hii ya zoezi la kuhamisha makaburi kipande cha Morogoro- Makutupora linahusisha wilaya za Kilosa na Dodoma ambapo zaidi ya Makaburi 500 yanatarajiwa kuhamishwa ili kupisha shughuli za Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa ikiwemo upasuaji miamba, uchimbaji udongo na maeneo kwa ajili ya ujenzi a stesheni.

Shirika linaendesha zoezi kwa kufuata taratibu za kisheria kwa kushirikisha wataalamu kutoka katika Vijiji/Mitaa/Vitongoji, Kata, Wilaya pamoja na Mikoa ambayo zoezi linafanyika sambamba na kuwapa uelewa wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi la kuhamisha makaburi katika Miradi ya maendeleo ukiwemo Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa.

Shirika linawashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa katika kufanikisha zoezi na linawaomba kuendelea kutoa ushirikiano ili mkandarai aweze kumaliza kazi ya ujenzi wa reli kwa muda uliopangwa.