Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​​ZAIDI YA KAYA 35 KULIPWA FIDIA MASWA MKOANI SHINYANGA


news title here
28
October
2021

Shirika la Reli Tanzania- TRC linaendelea na zoezi la ulipaji fidia kwa kaya zaidi ya 35 ambazo maeneo yao yalitwaliwa awali ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha tano Mwanza - Isaka , linalofanyika katika kata ya Seke Bugolo na kata ya Malampaka wilayani Maswa hivi karibuni Oktoba, 2021.

Zoezi hilo la ulipaji fidia ambalo linafanyika kwa ufanisi mkubwa, linaloongozwa na maafisa kutoka TRC pamoja wenyeviti na watendaji wa vijiji na vitongoji kwa lengo la kuhakikisha walengwa wote wanapewa malipo yao stahiki bila migogoro wala sintofahamu ya aina yoyote.

Afisa Ardhi kutoka TRC Bwana Valentine Baraza ameeleza kuwa maeneo hayo yaliyotwaliwa yatatumika kujenga kambi za mkandarasi, majengo ya ofisi , mabweni ya kulala, kumbi za mikutano, zahanati na sehemu za kuhifadhia vifaa vya ujenzi.

“Zoezi hili ni endelevu na imani yetu wananchi watatoa ushirikiano ili ujenzi uweze kwenda kwa kasi zaidi” alisema Bwana Baraza

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Seke Ididi Bw. Raymond Nyeye ameipongeza serikali pamoja na TRC kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao kwa wakati pamoja na kutoa elimu mbalimbali za maendeleo kwa wanakijiji kujua ni jinsi gani watatumia fidia hizo katika mambo muhimu ya kujiendeleza kiuchumi.

“Wanakijiji wanatoa ushirikiano mzuri bila malalamiko wala usumbufu wa aina yeyote “ alisema Bw. Nyeye.

Pia mkazi wa kijiji cha Seke Ididi Bw. Michael Martin ameishukuru sana serikali na Shirika la Reli Tanzania kwa kufuata sheria na kutenda haki ya kulipa fidia kwa kila mtu ambae eneo lake limetwaliwa , kwa kukagua nyaraka za mtu husika na pia nyaraka za mirathi.