Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

ZAHANATI YA TRC YA POKEA VIFAA TIBA


news title here
08
December
2023

Zahanati ya Shirika la Reli Tanzania - TRC imepokea vifaa tiba kutoka kwa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania kikosi cha reli kanda ya Dar es Salam ikiwa ni katika kuadhimisha Siku Kumi na Sita (16) za kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini iliyofanyika katika Zahati ya Reli ilioko Jijini Dar Es Salaam hivi karibuni , Disemba 08 , 2023.

Vifaa hivyo vilivo pokelewa ni pamoja na mipira ya kuvaa mikononi , pamba za kusafishia vidonda , mipira ya kutandika vitandani , tochi za kumulikia wakati wa uchunguzi , Sanduku la vifaa vya huduma ya kwanza , bandeji za kufungia vidonda , spiriti kwa lengo la kuwezesha zahanati hiyo kutoa matibabu fanisi ya kuokoa maisha na kupunguza maumivu kwa wagonjwa hasa kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.

Kaimu Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli Tanzania ASP Florence Mwenda alisema kuwa Zahanati hiyo ya reli ipo sehemu yenye mzunguko wa watu wengi wenye matumizi mengi ya vifaa vya moto na imekua mstari wa mbele katika kutibu wagonjwa wanaopata majeraha kutokana na ajali.

“Jeshi la Polisi kikosi cha reli limeona umuhimu wa kutoa msaada wa vifaa tiba ili kurahisisha na kusaidia katika matibabu” alisema ASP Mwenda.

Aidha ASP Mwenda alieleza kuwa wanawake ni kundi lenye umuhimu mkubwa katika kuchangia ukuaji wa uchumi na kuhakikisha malezi ya familia hivyo Jeshi la polisi kikosi cha reli limeona ni vema kuadhimisha siku hizo za upingaji na unyanyasaji wa kijinsia nchini zenye kauli mbiu isemayo “Wekeza katika kuzuia ukatili wa kijinsia”.

“Jeshi la polisi kikosi cha reli kimejizatiti katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa wanawake unapatikana na vilevile kuhakikisha inatokomeza ukatili huo katika jamii zetu” alisema ASP Mwenda.

Nae Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Bwana Hamphrey Kong’oke kwa niaba ya Shirika la Reli Tanzania amelipongeza Jeshi la Polisi Kikosi cha Reli kwa kutambua umuhimu wao katika jamii na kuweza kutoa msaada wa vifaa tiba katika kuboresha huduma za afya kwenye jamii.

“Pamoja na kwamba polisi wanapambana na ukatili , lakini wameamua kwa dhati kuisaidia hospitali ya reli ili iweze kusaidia walioathirika na kupata maumivu kutokana na majereha , ni jambo la faraja sana” alisema Bw. Kong’oke.

Mganga Mkuu Zahanati ya Reli Dk. Peter Mathew msaada a vifaa tiba katika hospitali ya reli vitaisaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto mbalimbali za utoaji huduma matibabu na kuweza kuwahudumia wagonjwa wa ufanisi Zaidi.

“Wateja ni wengi sana , majeruhi ni wengi sana haswa katika hiki kipindi cha mvua nyingi na mafuriko ukiangalia sehemu ilipo hospitali yetu , tunapokea wagonjwa wengi wanaletwa kutokana na ajali za pikipiki, magari na matattizo mengine ya kiafya “ Alisema Dk. Peter.

Ni vema Shirika na Nchi kiujumla kuwekeza katika kukomesha ukatili wa kijinsia unaondelea kufanyika hasa kwa wanawake hiyo italeta matokeo chanya ya kimaendeleo katika jamii.