WAWAKILISHI WA WAJUMBE WA KAMATI YA MADENI YA KITAIFA WAFANYA ZIARA KATIKA MRADI WA SGR

April
2019
Wawakilishi wa Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Madeni watembelea kambi za Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR, Ilala na Soga kipande cha Dar - Moro kwa lengo la kuona maendeleo ya Mradi mwanzoni mwa Aprili 2019.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Reli TRC Mhandisi Felix Nlalio, Meneja Msaidizi Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Mhandisi Ayoub Mdachi, wawakilishi walipata fursa ya kuona hatua tofauti za ujenzi wa reli ya kisasa – SGR ikiwemo ujenzi wa Stesheni, Madaraja, Makalavati pamoja na uzalishaji wa Mataruma ya reli katika kiwanda kilichopo kambi ya Soga Kibaha mkoani Pwani.
Aidha, akizungumza kwa niaba ya wawakilishi wa wajumbe wa Kamati Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bwana Omary Kama amesema kuwa wameridhishwa na wamefurahishwa na kasi ya ujenzi kwa sababu kazi kubwa imefanyika na inaendele kufanyika
Amesema Omary Kama “Ukiwa nje huwezi kujua kinachofanyika, kazi kubwa inafanyika, reIi inavutia kwa kuitizama na kazi kubwa imefanyika, niseme tu tumeridhishwa na tumefurahishwa na maendeleo ya mradi”
Moja kati ya majukumu ya Kamati ya Madeni ya Kitaifa ni Kuchambua Miradi ya kitaifa ukiwemo Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR na kuitafutia fedha ili Miradi iweze kukamilika ndani ya muda uliopangwa.