Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​MIUNDOMBINU YA SGR IKO SALAMA - RC CHALAMILA


news title here
12
December
2025

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, amewahakikishia wananchi na raia wa kigeni kuwa miundombinu ya SGR iko salama kwa upande wa Dar es Salaam na kipande chote cha reli mpaka Dodoma na kutoa rai kwa abiria kutohofia hivyo wandelee kutumia huduma zitolewazo na TRC.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, ametoa kauli hiyo Desemba 12,2025 alipotembelea jengo la stesheni ya Magufuli la SGR lililopo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kiutendaji ambapo amejionea huduma zinazotolewa na TRC pamoja na kuzungumza na abiria wanaosafiri kati ya Dar es Salaam na Dodoma, Pamoja na wafanyabiashara waliowekeza ndani ya steheni ya Magufuli.

Aidha katika ziara yake hiyo, amezungumza na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Machibya Shiwa Pamoja na menejimenti ya TRC juu ya amsuala kadhaa ikiwemo weledi wa wafanyakzi na kusikia utayari wa TRC kwenye swala la ujenzi wa reli za mijini.

“Tunawathibitishia miundombinu ya TRC pamoja na mambo mengine yote iko salama na tutaendelea kuilinda kwakua ina maslahi makubwa kwa kila mmoja” alisema Mhe. Chalamila.

Kuhusiana na ulinzi wa miundombinu ya SGR, Mhe. Chalamila, ameeleza kuwa wakuu wa Mikoa wote kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma wamekua na vikao vya pamoja ili kuhakikisha kunakua na usalama katika korido zote ambazo miundombinu ya reli ya SGR inapita.

“Korido zote ambako miundombinu ya reli inapita inahitaji ulinzi shirikishi wa viongozi na wananchi kwa ujumla ili uwekezaji huu mkubwa uendelee kubaki salama” alisisitiza Mhe. Chalamila.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Machibya Shiwa, alisema kuwa TRC imekamilisha hatua za awali za upembuzi ujenzi wa mradi wa reli za mjini kama Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyotoa maelekezo kwenye hotuba na ahadi zake wakati wa uchaguzi.

“Sisi kama TRC tumeshajipanga na tunaenda kwenye hatua ya pili ya ujenzi wa mradi wa reli za mjini na ifikapo mwakani tutaanza hatua ya ujenzi wa reli za mjini hivyo TRC itahakikisha kuwa reli hizo zinajengwa” alieleza Mhandisi Machibya.

Wakati huo huo Mhandisi Machibya, amesema, TRC itaendelea kuhakikisha inaboresha miundombinu ya reli pamoja na huduma zitolewazo kwa ubora na kuzidi kudumisha usalama katika maeneo yote ya korido ya miundombinu ya reli.