Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WANANCHI WAMSHUKURU MH. RAIS JPM KWA KULIPWA FIDIA KWA WAKATI WALIOPITIWA NA UJENZI WA SGR


news title here
21
May
2020

Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na zoezi la ulipaji Fidia kwa wananchi waliopitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR mkoani Dodoma Hivi karibuni Mei ,2020.

Zoezi hilo la ulipaji Fidia limefanyika kwa Siku mbili tarehe 18 - 19 Mei ambapo wananchi zaidi ya 87 wa Mtaa wa Bahi Mapinduzi wamelipwa fidia zao za ardhi na makazi ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 68 zimelipwa kwa wananchi wa mtaa huo.

Wananchi wa Mtaa wa Bahi Mapinduzi wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na TRC kwa kufanikisha zoezi hilo licha ya kuwa na chagamoto ya ugonjwa wa Corona inayoikabili Dunia hivi sasa ambapo Uchumi wa Dunia umeshuka kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Bahi Bwana Joseph Mayonde Mkwawa ameishukuru TRC na Serikali ya awamu ya tano kwa kulipa fidia kwa wananchi wa Mtaa huo na kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa Maafisa wa TRC na Viongozi wa Mtaa na Kata ambao wamekuja ili kufanikisha Zoezi hilo kwa muda uliopangwa.

Mtendaji wa Kijiji Bwana Legnado Ndahani wa Bahi Mapinduzi ameipongeza TRC kwa kuzingatia hatua za kupambana na ugonjwa wa Corona kwani wamelipa kwa Siku mbili watu wachache wachache hivyo amewashukuru sana TRC na maafisa waliokuja kwa ajili ya zoezi hilo.

Bwana Yusuph Mrisho Mhasibu TRC amesema "Hundi zote ambazo wananchi wamepewa hawapaswi kuziandika ama kuzichafua, Hundi zinaweza kukaa miezi 6 baada ya tarehe ya kuandikwa, hivyo wananchi mnatakiwa kuzipeleka Benki husika mapema ili kuepusha usumbufu ambao unaweza kutokea pia amewaasa wananchi wawe makini na matapeli hasa katika kipindi hiki cha kulipa Fidia.

Shirika linaendelea kutoa Rai kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikano katika Zoezi hili la Ulipaji Fidia bila kukwamisha ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli.