Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WANANCHI WALIPWA FIDIA KUPISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME SGR MKOANI MOROGORO


news title here
15
November
2022

Shirika la Reli Tanzania limelipa fidia kwa wananchi wa kijiji cha Lukobe Juu mkoani Morogoro katika kipande cha pili Morogoro - Makutupora, Novemba 2022.

TRC imelipa jumla ya hundi 14 kwa wananchi kwa lengo la kupisha eneo la mradi wa ujenzi wa miundombinu ya umeme kwaajili ya Reli ya kisasa awamu ya pili katika kijiji hicho wilaya ya Morogoro.

Mpimaji Ardhi kutoka TANESCO Bwana Derick Kaijanangoma amewaomba wananchi waliopatiwa hundi zao kufuata taratibu za kuachia maeneo ili kuipa nafasi TANESCO kujenga miundombinu ya umeme ili kufanikisha mradi wa SGR katika kipande hicho.

Wananchi wameishukuru TRC na Serikali kwa kuzingatia malipo yao kulipwa kwa wakati hivyo kuwawezesha kununua ardhi sehemu nyingine ili kupata mahitaji muhimu ikiwemo kujenga nyumba na kuwekeza katika biashara.

Mtendaji wa Mtaa wa Lukobe Juu Godfrey Dipruti Mushi amewapongeza wananchi wake kwa kuonesha ushirikiano kwa TRC na TANESCO muda wote wa uthamini hadi kufikia malipo ya hundi.

Shirika la Reli Tanzania linawapongeza na kuwashukuru wananchi wanaoendelea kupisha maeneo yao kwaajili ya muendelezo wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa vipande vyote vinavyojengwa.