Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WANANCHI WA KATA YA IHUMWA WAENDELEA KULIPWA FIDIA ILI KUPISHA UJENZI WA RELI YA KISASA


news title here
16
June
2020

Shirika la reli Tanzania -TRC laendelea na ulipaji wa fidia kwa wananchi 164 wa Kata ya Ihumwa jijini Dodoma hivi karibuni

Fidia hizo zinatolewa kwa wananchi mara baada ya Shir.ika la Reli Tanzania – TRC kutwaa rasilimali zao kwa lengo la kupisha ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kwa awamu ya Pili Morogoro – Makutupora, ambapo zoezi hilo ni endelevu kwa sasa linaendelea kufanyika Mkoani Dodoma katika kata ya Ihumwa.

Aidha, Kutokana na sera na sheria za ardhi ambayo inabainisha kuwa, fidia ni malipo yanayotolewa kwa mtu au taasisi kama mbadala wa mali yake kutokana na kuondolewa kwenye eneo lake lililotwaliwa kwa manufaa ya umma na kupangiwa matumizi mengine tofauti na yale yaliyopo kwa sasa.

Kwa hali hii inadhihirisha dhahiri Miradi inayosimamiwa na TRC imeletwa kwa lengo la kuleta faida kwa wananchi wa Tanzania hivyo serikali inawajibika kulipa fidia, kupitia Shirika la Reli nchini.

TRC imetenga kiasi cha fedha za kitanzania 254,725,292/= ili kuwalipa fidia wananchi wa Kata ya Ihuwa na kuwataka punde tu wanapopokea hundi ya malipo kupisha maeneo ndani ya siku 14 na mkandarasi kuendelea na ujenzi wa reli.

Katika hatua nyingine, maelfu ya wakazi wa Dodoma wanaendele kupokea stahiki zao za fidia ambazo kwa wengi imekuwa ni fursa na njia ya kubadilisha na kuboresha maisha yao kutokana na kwamba fedha hizo zinapotolewa kwa wananchi kitengo cha mambo ya jamii kutoka Shirika la Reli pamoja na Viongozi wa ngazi ya kata mpaka Mkoa hutoa elimu juu ya matumizi bora ya fedha wanazolipwa hasa katika kuleta tija katika maendeleo ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, wananchi wametoa shukurani kwa Serikali na Shirika la Reli kwa kutimiza ahadi ya kulipa fidia ambayo kwa muda mrefu walikuwa wakisubiri, kwa upande mwingine wananchi wameonesha kufurahia mradi huo kwani umekuwa ni fursa kwa wakazi wa maeneo hayo ambapo vijana wa kike na wakiume wamejipatia ajira mbalimbali huku wengine wakijikita katika fulsa ya biashara ndogondogo na ndoto kubwa ikiwa punde tu mradi utakapokamilika na kuanza kazi itakuwa ni fulsa kwao na kwa maendeleo ya mji wa Dodoma hasa katika kukuza uchumi wa ngazi ya familia mpaka ngazi ya Taifa.