Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WANANCHI TAKRIBANI 250 WALIPWA FIDIA KUPISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SGR KIPANDE CHA PILI MOROGORO - MAKUTOPORA


news title here
20
October
2023

Shirika la Reli Tanzania limelipa fidia kwa wakazi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR kipande cha pili Morogoro - Makutopora Oktoba, 2023

Wananchi takribani 250 wamelipwa fidia katika wilaya ya Dodoma Mjini, Bahi, Mpwapwa na Chamwino jijini Dodoma, wananchi wengine waliolipwa fidia ni wa wilaya ya Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro na bandaye walilipwa fidia wananchi wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Afisa ardhi kutoka TRC Benlulu Lyimo amesema maeneo yaliyolipwa fidia ni kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miundombinu ya umeme na vivuko kwenye reli ya kiwango cha kimataifa.

"Fidia inayolipwa ni kwa mujibu wa Sheria, kanuni na Taratibu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzanian" alisisitiza Bi. Benlulu

Mtendaji wa Kata ya Mkonze wilaya ya Dodoma Mjini Bw.Matonya Kaondomo ameishukuru serikali na TRC kwa kulipa fidia kwa wakati ili wananchi wapishe ujenzi wa miundombinu ya reli ya SGR

"Wananchi wenzangu, fedha hizi mnazolipwa mkanunue maeneo mengine ili muone faida ya mradi" alisema Bw. Matonya

Bwana Richard Stephen mkazi wa mtaa wa Muungano B kata ya Mkonze wilaya ya Dodoma Mjini ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuwalipa fidia kwa kiwango walichokuwa wakikitarajia.

"Eneo langu nilikuwa nalima mazao ya chakula, haya malipo niliyopokea nakwenda kununua eneo lingine" alisema Bw. Richard.

Zoezi la ulipaji fidia ni endelevu ili kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya SGR inakuwa ya kiwango cha kimataifa.