Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WANANCHI KATA YA NGETA, RUVU MINAZI MIKINDA WAISHUKURU TRC KWA ULIPAJI WA FIDIA


news title here
01
September
2020

Wananchi wa kata ya Ngeta na Ruvu Minazi Mikinda waishukuru Shirika la Reli Tanzania - TRC kwa kulipwa fidia za makazi na ardhi mkoani Pwani Agosti 31, 2020.

Wananchi wa kata hizo wamelipwa fidia zao ili kupisha Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR ambao mpaka sasa unakaribia kukamilika kwa Kipande cha Dar es Salaam - Morogoro.

Zoezi hilo limefanywa na Maafisa toka Shirika la Reli kwa kushirikiana na watendaji wa kata za Minazi Mikonda na Ngeta ambapo watendaji kata husika wameshiriki kikamilifu kwa kuhakikisha zoezi zima linamalizika kwa wakati na wananchi wote ambao maeneo yao yametwaliwa wanalipwa fidia zao kama walivyoahidiwa.

Mmoja wa Wananchi waliolipwa fidia, toka kata ya Ruvu Minazi Mkinda Bi Hawa Selemani amewashukuru TRC pamoja na Serikali ya awamu ya Tano kwa kupewa fidia zao “tetesi zilikuwa nyingi mno mpaka tulikuwa kila siku hatukauki kwenye ofisi ya kata kumsumbua mwenyekiti na Mtendaji kwani tulihisi wanakula njama na TRC ili tucheleweshwe kulipwa fidia zetu ila Mungu ni mkubwa leo tumelipwa fidia ambazo hata wengi wetu hatukuwaza kama zingekuwa kubwa hivi” alisema Bi. Hawa .

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Ngeta Bi. Mwanahisi Rajabu amelishukuru Shirika la Reli na kuomba kumalizia kulipa fidia kwa wale walikutwa na changamoto na kushindwa kulipwa kwa sasa ili kuondoa usumbufu na wananchi waweze kuendelea na Maisha yao ya kila siku ya ujenzi wa taifa ukizingatia nchi ipo kwenye uchumi na kati na Mradi wa Ujenzi ya Reli ya Kisasa unapita kwenye maeneo haya natengemea wananchi wa Kata ya Ruvu Minazi Mikinda na Ngeta watajiongeza kwa kufanya biashara ili kuendelea kuwa kwenye kipato cha kati na kuunga jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu wa tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, sisi watendaji wake tuko nae bega kwa bega kuhakikisha tunampa ushirikiano wa Kutosha.

Halikadhalika Kwa upande wake Afisa Ardhi kutoka TRC Bwana Valentine Baraza amewasihi wananchi wa kata hizo kuchukua hundi hizo hata kama wanaona wamelipwa kidogo ili baada ya kuchukua waandike barua kwa TRC kulalamika na changamoto zozote zilizotokea na TRC itashughulikia Changamoto hizo mara moja wapatapo malalamiko hayo.

Maria Machungwa Mtaalamu wa Masuala ya Kijamii amewatoa hufu wananchi wa Kata hizo na kusema “sisi maafisa jamii wa TRC tupo kwa ajili yenu tutashughilikia changamoto zote ambazo zinawakuta katika kipindi chote hiki cha Mradi, Ofisi yetu ipo wazi mnakaribishwa na tuna namba ya bure ambayo iko hewani saa 24"

Wananchi wa kata ya Ruvu Minazi Mikinda na Ngeta wameishukuru TRC na Serikali kwa kukamilisha fidia zao na kuahidi kuwa mradi wa SGR utakapoanza kufanya kazi watahakikisha ulinzi wa Miundombinu hiyo na kuchangamkia fursa za kiuchumi zitakazojitokeza.