Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WANANCHI BAHI MKOANI DODOMA WALIPWA FIDIA KUPISHA MRADI WA SGR


news title here
21
November
2021

Shirika la Reli Tanzania - TRC limeendelea na zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi waliotwaliwa maeneo yao kupisha ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa katika Kijiji cha Bahi Sokoni na Bahi Makulu mkoani Dodoma Novemba 2021.

Katika zoezi hilo la ulipaji fidia kwa wananchi TRC imelipa zaidi ya shilingi Milioni 102 kwa kaya 23 , zikiwemo kaya 17 kwa Kijiji cha Bahi Sokoni na kaya 6 kwa Bahi Makulu mkoani Dodoma kwa ajili ya kupisha eneo la kiwanda cha kuponda kokoto kilichopo kijijini hapo..

Mwenyekiti wa Bahi sokoni Bwana Sifaeli Abel Mbeti amelishukuru Shirika la Reli kwa kuweza kulipa fidia kwa waathirika kwa wakati na kufuata utaratibu wa ulipaji fidia.

"Napenda kutoa pongezi kwa timu nzima ya TRC kwa kuhakikisha ulipaji wa fidia umekwenda vizuri na kwa wakati, wananchi wa kijiji cha Bahi wamefurahishwa na mfumo huu na wana imani kubwa na TRC" amesema Mtendaji wa Kijiji Cha Bahi Makulu.

Naye Bwana Mahembo Mathias Ndeki mkazi wa Bahi Makulu ameipongeza Serikali pamoja na TRC kwa kufanikisha ulipaji wa fidia kwa kuzingatia haki na sheria za malipo, vilevile amewashukuru viongozi wa kijiji cha Bahi Makulu kwa kuweza kuwapa ushirikiano tangu mwanzo wa uthamini wa ardhi Hadi kufikia malipo Novemba 2021.