Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WANAKIJIJI MKADAGE: TUTALINDA MIUNDOMBINU YA RELI


news title here
09
July
2020

Shirika la Reli Tanzania TRC limendelea na kampeni ya ushirikishwaji wa jamii katika maendeleo ya mradi wa uboreshaji wa reli ya kati kuanzia Kilosa hadi Isaka , Julai 2020 hivi karibuni.

Maafisa wa maswala ya jamii, wakandarasi kutoka kampuni ya CCECC, pamoja na wafanyakazi wengine kutoka TRC wametembelea maeneo mbalimbali yanayopitiwa na mradi huo ili kufahamisha umma kuwa mradi huo unakaribia kufika ukingoni hivyo kushirikisha wananchi katika kuweka mambo sawa kabla ya ukarabati kukamilika.

Maeneo yaliyofanyika kampeni hiyo ni pamoja na Kilosa kijiji cha Munisagara , Mkadage , Kilosa stesheni, Kidete na pia Zuzu stesheni, Mnase, Igangu , Kikombo , Godegode vilivyopo mkoani Dodoma.

Aidha wananchi wa kijiji cha Mkadage pamoja na viongozi wa Serikali ya kijiji hicho wameahidi kuilinda miundombinu na mali za reli katika maeneo yao na kusisitiza kua mtu yeyote atakae kiuka taratibu za reli atachukuliwa hatua na kufikishwa sehemu husika.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mkadage Bw. Mohammed Kikologa amesema kuwa kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji hicho watasimamia wanakijiji pamoja na kutoka elimu juu ya kutunza miundombinu ya reli .

“Sisi ndio walinzi wa kuu wa reli hii ila kukumbushana ni wajibu” alisema Bw. Kikologa.

Afisa wa maswala ya jamii kutoka CCECC Bw. Regan Israel amesisitiza kuwa mwananchi yeyote ahakikishe kutosogea ama kufanya shughuli za kijamii karibu na umbali wa mita zilizopimwa kando mwa reli .

“Mita zilizopimwa ni 30 kutoka katika eneo la njia ya reli “ , akaongezea kuwa “ ukiona mtoto, mzee au mtu asiyejiweza mshike mkono na umsaidie kuvuka “ alisema Bw. Regan .

Naye Afisa mazingira kutoka TRC Bw. Evance Byarushengo amewataka wananchi kutojihusisha na maswala ya ukataji miti na shughuli za kilimo kando ya mito ili kuepusha athari zitokanazo na maji kujaa na kuisomba miundombinu ya reli