Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WANAJESHI KUTOKA NCHI ZA AFRIKA WATEMBELEA MRADI WA SGR


news title here
09
April
2021

Wanajeshi kutoka nchi mbalimbali za Afrika walio katika mafunzo ya kubadilisha ujuzi watembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) tarehe 9/04/2021.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuona maendeleo ya mradi wa SGR unaondelea nchini .
Ziara hii iliyoratibiwa na Jeshi la wananchi la Tanzania ilijumiuisha wanajeshi kutoka nchi Uganda , Kenya, Sudan Kusini, Rwanda , Burundi, India na Afrika Kusini.
Aidha katika kueleza nia ya ziara hiyo ,Mkurugenzi wa Idara Miundo Mbinu kutoka Shirika la Reli Tanzania(TRC) Muhandisi Faustine Kataraiya, ameeleza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujifunza jinsi miundo mbinu ya Reli inavyojengwa, kuendeshwa ,makusudio pamoja na maligafi zinazotumika katika ujenzi wa reli ya kisasa.“Kama unavyowaona hao ni wanafunzi ,pamoja na waadhiri wao na viongozi wao wameratibiwa na chuo cha mafunzo cha kwetu hapa Tanzania kupitia jeshi la Wananchi la Tanzania”Alisema Muhandisi Kataraiya.
Muhandisi Kataraiya aliongeza kuwa katika ziara hiyo maalumu wanajeshi hao wamefanikiwa kufahamu hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huu wa SGR kwa awamu hii ya kwanza kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, ambao ni jumla ya kilomita 1219 kilomita na hadi sasa kipande kutoka Dar Es Salaam mpaka Morogoro ushakamilika kwa asilimia tisini(90%) na kutoka Makutupora Mpaka Singida umefikia asilimia sitini(60%) na kipande cha tano kutoka Mwanza mpaka Isaka ushaanza ambao utakutana na kipande cha kutoka Makutopora mpaka Singida.
Katika Majumuisho ya ziara hii, Muhandisi Kataraiya pia alieleza jopo hilo nia ya Shirika la Reli Tanzania azma yake ya kuendeleza ujenzi huu wa reli ya kisasa hadi kuziunganisha Nchi za Afrika Mashariki haswa zisizokuwa na bandari kama vile Uganda, Rwanda , Burundi na Demokrasia ya Kongo ili kuongeza wigo katika biashara na kuleta Mshikamano.“Tunampango wa kujenga awamu nyingine ukiacha hii ya kwanza ambayo ni Tabora mpaka Kigoma ambayo itaunganisha na Burundi na Isaka mpaka Rusumo na Kigali ambayo itatuunganisha na Rwanda,na hata Kusini Mwatanzania kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay ili kuunganisha bandari ya Mtwara na Malawi na Kilwa mpaka Bandari ya Kalemi kutuunganisha na nchi ya Kidemocrasia ya Congo(DRC).
Akitoa maelezo kuhusu swali aliloulizwa na mmoja wa wanajeshi katika ziara hiyo kuhusu changamoto za upatikanaji wa umeme miongoni mwa Nchi jirani amabazo Shirika la Reli linatarajia kuunganisha reli ya kisasa, Mkurugenzi wa idara ya ujenzi Muhandisi Kataraiya alitoa ufafanuzi wa jinsi gani shirika la Reli lilivyojindaa kushirikiana na shirika la ugavi wanishati ya umeme hapa nchini ili kuhakikisha mradi huu unaendelea kujengwa na kutoa huduma madhubuti.“Kutoka Dar Es Salaam mpaka Mkutupora miundombinu ya umeme wa mega wati 220 ishakamilika na Nchi ya Tanzania kupitia Shirika la Umeme Tanzania Tanesco ina mkakati wa kuzalisha umeme wa kutosha hata kuweza kuwasaidia majirani zetu ambao wanachangamoto hiyo,tuna mradi wa Nyerere Hydro power ambao unajengwa kusini mwa Tanzania ambao ukikamilika utazalisha Zaidi ya mega wati 2000, hizi zitatosha kabisa katika ujenzi huu .
Pia Makamu Mkuu wa Chuo na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Ukamanda na Unadhimu Bregedia Klavia Butoro kutoka Nchi Uganda alipata nafasi ya kuelezea lengo kuu ya ziara hii ni mafunzo ya kidiplomasia hasa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ili kudumisha ushirikiano na umoja na pia kujifunza mambo mbalimbali ya maendeleo.“kawaida tunafanya ziara hizi kubadilishana ujuzi ,na tutakapofika nyumbani tanaandaa ripoti ya haya yote tulioyaona na kujifunza na kupeleka kataika ngazi zinazohusika na maamuzi”Alisema kamanda Klavia Butoro Miungoni mwa vitu walivyojifunza ni pamoja na Uelewa wa miundombinu ya Reli Tanzania,Usanifu ,uzingatiaji wa ujenzi salama,Uhandisi wa Reli na Makapuni ya ndani yanavyoshirikishwa katika ujenzi.