Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WANAFUNZI CHUO CHA RELI TABORA WATEMBELEA MRADI WA SGR


news title here
05
September
2023

Wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia ya Reli Tabora - TIRTEC wanaosoma masomo ya usafirishaji, ujenzi na matengenezo ya reli na kozi mbalimbali kwa ngazi ya Stashahada na cheti watembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha Kimataifa kipande cha kwanza Dar es Salaam - Morogoro Septemba 5, 2023.

Makamu mkuu wa Chuo mipango fedha na utawala Bw. Edward Chezari amesema lengo la wanafunzi ambao wapo kwenye mafunzo ya vitendo ni kutembelea mradi ili kujifunza mambo yanayohusu ujenzi na uendeshaji wa treni za SGR kwa kuona mifumo mbalimbali ya kitalaam itakavyokua inafanya kazi pindi safari zitakapoanza pamoja na kuona mabehewa yatakayobeba abiria yaliyowasili nchini zikiwemo behewa za ghorofa.

"Wanafunzi wameona mfumo mzima wa control room (chumba cha kongozea treni) kutoka Dar es salaam hadi Makutupora utakaofanya kazi kupitia watalaamu watakavyofanya kazi kwenye chumba hicho" ameongeza Chezari

Rais wa chuo cha Reli Tabora Bi. Herieth Nelson amesema wamejifunza vitu vingi kuhusu mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa ikiwemo usafarishaji wa abiria, mizigo na wanyama utakavyokua hapa nchini sehemu ambazo SGR itapita.

"Kupitia ziara hii tumeweza kujua tofauti iliyopo kati ya reli ya MGR (reli ya zamani) ambayo ni reli inayotumia mafuta na inaweza kutembea kwa kutumia muda mrefu katika safiri tofauti na reli ya SGR ambapo inatumia umeme na itasafiri kwa kutumia mda mfupi na kwa haraka zaidi ameongeza Herieth.

Waziri wa Elimu kutoka chuo cha Reli Bw. Robert Pyakula ameishukuru menejimenti ya TRC pamoja na uongozi wa chuo kwa kuwapa nafasi ya kutembelea mradi kwani kupitia nafasi hii wamejifunza mambo mengi ya uendeshaji wa treni ya SGR na anapenda kuwakaribisha wanafunzi waliomaliza elimu za kidato cha nne na sita wajiunge na chuo cha reli Tabora pamoja na Morogoro ili waweze kupata taaluma inayohusu utaalamu wa masuala ya reli ili waweze kujiunga na Shirika la Reli Tanzania.

Ni takribani wanafunzi 35 wa Reli wametembekea mradi wa SGR, Chuo cha reli Tabora kinatoa kozi katika mitaala ya usafirishaji, ufundi wa mabehewa ya treni, ujenzi na matengenezo ya reli, ishara ya mawasiliano ya njia za umeme pia kuna chuo cha reli tawi la Morogoro kinachotoa elimu ya mitaala ya ufundi wa vichwa vya treni na udereva wa treni.