Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAFANYAKAZI WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO WATEMBELEA SGR


news title here
02
December
2020

Wafanyakazi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kutoka Dodoma mpaka Morogoro, hivi karibuni Novemba, 2020.

Aidha, lengo la ziara wafanyakazi wa Wizara hiyo ni kuja kuona hatua ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR ulipofika ili kuipa fursa Wizara yenye dhamana ya habari kuona na kushuhudia mradi huo ili kuwa na wigo mpana wa kuueleza na kuuhabarisha umma kuhusu hatua za utekelezaji kwenye mradi mkubwa ambao utakuwa na matokeo makubwa na utachangia kukua kwa uchumi wa nchi.

Ugeni huu umepokelewa na Meneja Mradi msaidizi SGR kipande Morogoro – Makutupora Mhandisi Christopher Mang’wela ambaye aliwaongoza wafanyakazi hao kutembelea mradi na kujifunza mambo mbalimbali katika ujenzi huku akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa. Mhandisi Mang’wela alielezea maendeleo ya mradi katika hatua mbalimbali za ujenzi huku akitoa nafasi ya maswali kwa wafanyakazi hao kwa lengo la kuwaelimisha ili kuwajengea uwezo wa kuusemea mradi vyema kwa umma.

Kwa upande wake Mkuu wa msafara Petro Lyatuu ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ameeleza namana alivyoo jionea na kuridhika kwa kasi na hatua kubwa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa.

‘’Ujenzi huu unahusisha mambo mengi, tumeona ujenzi wa madaraja ambao kwa asiliamia kubwa yamekamilika, pia utandikaji wa reli tunaona maeneo mengi reli imekwisha kutandikwa hata miundombinu ya umeme tumeona maeneo mengi nguzo zimekwisha kuwekwa. Hatua ambayo imefikukiwa ya utekelezaji ni hatua ya juu sana niseme tu kwamba hivi, karibuni watanzania wataanza kunufaika na mradi huu’’ Mkurugenzi wa Sera na Mipango alisema.

Mara baada ziara hiyo kufikia tamati katika eneo la Mkata mkoani Morogoro, Wafanyakazi hao wameeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi ikiwemo ujenzi wa stesheni za reli ya kisasa, utandikaji wa reli na mataruma na uwekaji wa miundombinu ya umeme samabamba na ujenzi wa vivuko. Katika hatua nyingine wafanyakazi hao waliishukuru Serikali kwa ajili ya mradi huu ambao umetengeneza ajira nyingi wakati wa ujenzi lakini pia walitoa pongezi kwa Shirika kwa kusimamia mradi huo kwa ufanisi huku ujenzi kipande cha Morogoro – Makutupora kwa ujumla ukifikia zaidi ya 40%.