Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​*WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RELI WAPATA MAFUNZO JUU YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORONA.


news title here
12
March
2020

Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania wapata mafunzo juu ya kujikinga na ugonjwa hatari la korona katika semina elekezi ya ugonjwa huo wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa umekua tishio duniani kote iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano TRC hivi karibuni machi, 2020.

Ugonjwa wa Corona ambao hadi sasa umesambaa katika nchi mbalimbali ikiwemo China ambapo ndipo ulipoanza kugundulika, umekua ukileta hofu kubwa kwa kuwa na maambukizi ya haraka kwa kupitia njia ya majimaji (jasho), pamoja na njia ya hewa.

Daktari kutoka Zahanati ya Shirika la Reli Tanzania- TRC Methew Peter ametoa mafunzo hayo kwa wafanyakazi wa shirika kwa upana Zaidi ili waweze kupata uelewa Zaidi wa kitaalam, na kusema kua ugonjwa huo ambao virusi vyake husambaa kwa kasi sana na kuwaasa wajiepushe kushikana mikono pamoja na kujishika sehemu za uso pamoja na kuwashauri wanawe mikono mara kwa mara.

Virusi hivyo vinasababisha homa kali sana kama nyuzi joto 38, kubanwa kwa mapafu na kukohoa pia husababisha mtu kushindwa kula kutokana na maumivu ya koo, alisema Dkt. Methew.

Hata hivyo alisisitiza juu ya njia za kuzuia njinsi ya kujikinga na ugonjwa huo ambapo aliwaasa watu kuwa na usafi wa hali ya juu pamoja na kujiepusha swala la kusalimiana kwa kukumbatiana na kukaa karibu na msongamano wa watu wengi.

Nae Daktari Claudia Makanga amesema kuwa ni vizuri watu kufuata hatua za unawaji wa mikono kwa usahihi ambapo hatua hizo ni pamoja na kunawa mikono kwa kutumia maji yanayotiririka, kutumia sabuni, kusugua mikono kwa pamoja, kusugua sehemu za vidole,kusafisha kati ya vidole gumba na shahada, kusafisha kucha kwa kusugua kwenye viganja , pamoja na kutumia taulo kufunga mfereji kisha kutumia taulo nyingine kwaajili ya kujikausha.

Pia mafunzo hayo yamegusia pia watu ambao wanauguza tayari wagonjwa majumbani kwa kuwa waangalifu juu ya usafishaji wa vyombo anavyotumia mgonjwa mwenye Corona pamoja na usafishaji wa nguo anazotumia kwa kuzisafisha vizuri kwa kutumia dawa ambayo inauwa vijidudu kwa haraka.

Naye Mtaalam wa Maabara Ndugu. Alex Kudeli ameshauri watu kuwa na taratibu ya matumizi ya gloves katika shughuli tofauti za majumbani ambazo huepusha kwa kiasi kikubwa kukumbana na kushika bakteria ama uchafu utakaopelekea maambukizi kwenye mikono.

Mganga wa Zahanati ya Reli - TRC aliwashukuru wafanyakazi wa Kwa mwitikio mkubwa na kusisitiza kujikinga na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya ugonjwa huo kabla ya kufika nchini Tanzania.