Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WAFANYAKAZI 14 WA TRC KWENDA KOREA KUSINI KWA MAFUNZO YA SGR KWA VITENDO


news title here
26
November
2022

Shirika la reli Tanzani - TRC kupeleka wafanyakazi kumi na wanne (14) nchini Korea Kusini kwaajili ya mafunzo kwa vitendo kuhusu uendeshaji wa reli ya kisasa – SGR, Novemba 2022.

Mkurungenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kadogosa amesema mafunzo hayo ni utekelezaji wa mkataba wa mafunzo kwa vitendo uliosainiwa tarehe 4 Julai, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Shirika la reli Tanzania na Shirika la reli la Korea Kusini - KORAIL

Ndugu Kadogosa amesema wafanyakazi arobaini na tano (45) wanapatiwa mafunzo ya nadharia hapa nchini ili kuwajengea uwezo katika uendeshaji wa treni ya kisasa na sasaTRC inapeleka wafanyakazi kumi na nne (14) Korea kusini ili kupatiwa mafunzo kwa vitendo katika uendeshaji wa treni ya kisasa.

Ndugu Kadogosa ameongeza kuwa mafunzo yatatolewa nje ya nchi kwa wafanyakazi kumi na nne (14) kwa muda wa miezi mitano (5) kuanzia tarehe 1 Disemba 2022, mafuzo hayo yatakuwa katika kada ya Uendeshaji, Usalama wa reli, Miundombinu ya reli (Ujenzi, Ishara, Mawasiliano na Umeme) kada nyingene ni biashara, TEHAMA na mitambo.

“Korea Kusini wako mbele kwenye Technologia ya uendeshaji wa treni za kisasa mkajifunze kwa bidii na mtambue bado nyie ni watumishi wa umma na mnatuwakilisha huko nje ya nchi, tukipata taarifa za utovu wa nidhamu mtachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma” amesisitiza Kadogosa.

Mmoja wa watumishi watakaoshiriki mafunzo hayo Mhandisi wa Usalama wa reli Bwana Chisondi Maingu ameishukuru Serikali na Shirika kwa kuwaamini na kuwateua kushiriki mafunzo hayo na kuahidi kwamba watajifunza kwa bidii ili wapate ujuzi utakaowawezesha kusimamia vema uendeshaji wa reli ya kisasa na kuwafundisha watumishi wengine pindi watakaporejea nchini.