USAFIRI WA SGR KUONGEZA THAMANI YA MNYORORO WA UTALII ZANZIBAR
July
2026
Shirika la Reli Tanzania limelenga kuunganisha watu, biashara na fursa za kiuchumi kupitia reli ya SGR Zanzibar.
Reli ya SGR imetajwa kuwa moja ya miundombinu muhimu ambayo itaongeza Kasi za safari za watalii, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Zanzibar kwenda maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamekuwa sehemu ya mjadala katika Kongamano la Kuunganisha Uchumi wa Buluu, Biashara, Utalii na Fursa za Uwekezaji kupitia Reli ya SGR( Blue Economy, Trade, Tourism and Investment Opportunities Linkage to SGR) lililofanyika Zanzibar Julai 30, 2026.
Mtalii anapokuja Zanzibar ufurahia Mchanga wa Fukwe ( Sand), Jua ( Sun), Bahari ya Buluu ( Sea) na sasa kifungashio Cha nne ni Safari kupitia SGR ambapo mtalii atatembelea vivutio vya Tanzania Bara kama mbuga za wanyama na miji ya kihistoria .
Kwa upande mwingine Zanzibar itanufaika kupitia ongezeko la watalii wanaofika Tanzania Bara kama lango kuu la kuingilia visiwani huku wadau wa sekta ya hoteli, kampuni za utalii, wasafirishaji , waongoza watalii, migahawa na watoa huduma wakipata soko pana zaidi.
Kwa upande wa TRC imesisitiza sekta binafsi kuchangamkia fursa zilizopo kupitia ujenzi wa mradi huu wa kimkakati wa SGR ikiwemo kilimo, madini, uvivuvi, ujenzi wa viwanda na utalii ili kuongeza tija katika maendeleo ya nchi.
Ikumbukwe kuwa licha ya reli ya SGR kutofika Zanzibar bali itaimarisha Muunganiko usio na vikwazo kati ya SGR na mifumo mingine ya usafiri,
Mfano uratibu wa ratiba maalumu ya kusafirisha watalii, mifumo ya tiketi na taarifa za safari, huduma za usafiri kutoka vituo vya SGR kwenda bandarini au viwanja vya ndege na vifurushi vya utalii vinavyounganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

