Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

UCHORONGAJI MILIMA KWA AJILI YA UJENZI WA MAHANDAKI YATAKAZOPITISHA RELI YA KISASA YAENDELEA KWA KASI


news title here
30
August
2019

Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na usimamizi wa Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR Kilosa mkoani Morogoro, ambapo kazi kubwa katika eneo hilo ni uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki ‘tunnels’ yatakayopitisha reli ya Kisasa kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Milima ya Kilosa na Mto Mkondoa mkoani Morogoro, hivi karibuni Agosti 2019.

Mahandaki 4 yenye jumla ya urefu wa KM 2.6 yanatarajiwa kujengwa katika Mradi wa SGR kipande chaMorogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa huku handaki refu zaidi nchini likiwa na urefu wa KM 1.031 ili kuepuka athari za mto Mkondoa ambao umekuwa ukifurika kipindi cha mvua kubwa na kuathiri miundombinu ya reli ya ‘Meter Gauge’.

Hata hivyo ujenzi wa awamu ya pili ya reli ya SGR kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutupora Mkoani Singida, ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 14, huku kazi ya kuandaa tuta na madaraja ikiendelea lakini kubwa zaidi ni kazi ya uchorongaji wa mahandaki yapatayo manne, likiwemo hili lenye urefu wa kilomita moja.

Mhandisi Amiri Khamis Mkaguzi wa mahandaki kutoka Kampuni ya Korail Joint Venture ambao ni washauri wa ujenzi wa mradi amebainisha kuwa kazi ya uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki inaendelea kwa kasiambapo zaidi ya Mita 16 huchorongwa kwa siku. Mpaka sasa zaidi ya mita 200 kati ya Mita 1031 zimekwisha chorongwahuku kazi ya uchorongaji ikiwa imefikiazaidi ya asilimia 20. Aidha, kazi ya ujenzi wa mahandaki inatarajiwa kukamilika mwishoni mwamwaka 2019.

Naye Bi. Catherine Kipeja Mtaalamu kitengo cha kuangalia ubora wa kazi katika ujenzi wa handaki amezungumzia namna kazi ya ujenzi inavyofanyika kwa uhafanisi na kwa kuzingatia ubora hasa wa zege linalotumika kwenye ujenzi wa handaki hilo. “ kazi yetu kubwa ni kupima ubora wa zege, hasa tunapima joto la zege ambalo linatakiwa lisizidi nyuzi joto 32, mmiminiko wa zege usiwe chini milimita 100 ndipo mhandisi huruhusu gali la zege lipelekwe ndani” alisema Bi. Catherine.