Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YALIPA FIDIA WALIOPISHA NJIA YA UMEME SGR DODOMA NA SINGIDA


news title here
28
May
2022

Shirika la Reli Tanzania limefanya malipo ya fidia katika kipande cha pili cha mradi wa reli ya Kisasa SGR Morogoro - Makutopora katika wilaya ya Bahi mkoa wa Dodoma na Manyoni mkoani Singida mwezi Mei 2022.

Malipo hayo yamefanyika kwa wananchi waliotwaliwa maeneo yao kwaajili ya kupisha eneo la ujenzi wa njia ya umeme wa SGR katika kipande cha Morogoro - Makutupora.

Fidia zimelipwa kwa wanakijiji wa vijiji vya Nagulo, Mzogole na Kigwe wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, vilevile katika kijiji cha Lusilile wilaya ya Manyoni - Singida na wakazi hawa wote waliolipwa fidia wamepisha njia ya umeme.

Mthamini Ardhi Halmashauri ya Bahi Bi. Nuru Salei amesema wananchi walipewa elimu kabla ya maeneo yao kutwaliwa na vilevile walipatiwa elimu ya uthaminishaji ardhi na kufikia mariadhiano ya kuachia maeneo ili kupisha miundombinu ya umeme katika maeneo hayo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mzogole Bwana John Nzala amewapongeza wananchi wake kwa kuonesha utulivu kuanzia uthamini wa ardhi hadi kufikia malipo.

"Vilevile naishukuru TRC na Serikali kwa kupitisha reli ya SGR kijijini kwetu kwani itatusaidia kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kusafirisha bidhaa za biashara kwa wakati pamoja na kuturahisishia usafiri kwenda Dar es salaam na Morogoro" John Nzala alisema.

Mpimaji Ardhi kutoka Shirika la Umeme Nchini - TANESCO kanda ya kati Alphonce Mwandu amepongeza zoezi la ulipaji fidia pia amewapongeza wananchi kwa kuweza kutoa maeneo yao kupisha ujenzi wa miundombinu ya umeme kwaajili ya kufanikisha mradi wa reli ya Kisasa mkoani Dodoma uendelee.