TRC YALIPA FIDIA KWA WANANCHI WALIOPISHA MRADI WA SGR, MOROGORO

May
2022
Shirika la Reli Tanzania - TRC limeendelea na ulipaji fidia kwa wananchi waliotwaliwa maeneo yao kupisha upitishaji wa miundombinu ya reli ya Kisasa - SGR mkoani Morogoro, Mei 2022.
Wananchi wa Manispaa Morogoro na Morogoro Vijijini wamelipwa fidia kwa ajili ya kupisha upanuzi wa maeneo ya ziada kwaajili ya mradi, sehemu ya kuchimba na kumwaga kifusi na sehemu ya kituo kidogo Cha kupozea umeme.
Wananchi waliopokea fidia ni pamoja na 10 katika kata ya Tungi, 6 kata ya Azimio, 8 kata ya Lukobe, 4 kata ya Seminari, 6 kata ya Yespa 6, 1 kata ya Kilimanjaro na 5 katika kata ya Kihonda Kaskazini katika Manispaa ya Morogoro.
Pia TRC imelipa fidia kwa wananchi wilaya ya Morogoro vijijini ambapo wakazi 4 wa kata ya Mgude, 3 kata ya Mtego wa Simba, 1 kata ya Kinonko na 7 katika kata ya Mikese wamelipwa fidia zao.
Vilevile fidia ililipwa kwa wananchi 3 mkoa wa Pwani katika kijiji cha Kidugalo na wananchi 4 katika wilaya ya Mvomero kijiji Cha Kimambila.
Mthamini wa Ardhi Manispaa ya Morogoro Hassan Omary Mwanri amepongeza zoezi zima la ulipaji wa fidia kwasababu toka mwanzo wa uthamini wa Ardhi wananchi walishirikishwa na wakafikia mariadhiano.
"Naipongeza TRC kwa kukidhi vigezo vyote vya ulipaji fidia kwa wananchi na kufuata haki zote za msingi dhidi ya matakwa ya wananchi waliotwaliwa maeneo yao".
Naye mkazi wa Lukobe Bwana Cheni Pius Ambrose ameishukuru Serikali na Shirika la Tanzania kwa kuweza kulipa fidia kwa wananchi waliotwaliwa maeneo yao.
"Pesa hii inaenda kuniwezesha kufanya shughuli zangu na vilevile wenzangu wataweza kununua maeneo na kujenga kwa kupitia pesa walizolipwa na TRC".