Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YALIPA FIDIA KIJIJI CHA ISABILO WILAYANI KWIMBA - MWANZA


news title here
13
March
2022

Shirika la Reli Tanzania - TRC limeendelea na zoezi la ulipaji fidia katika kipande cha tanno cha reli ya kisasa - SGR katika kijiji cha Isabilo Kwimba mkoani Mwanza, Machi 2022.

TRC imelipa fidia kwa wakazi wa Kijiji cha Isabilo wilayani Kwimba mkoani ili kupisha mradi wa SGR, takribani wananchi 66 wamelipwa fidia kijijini hapo.

Afisa Ardhi wa Wilaya ya Kwimba Bwana Elias Gunze amesema wananchi waliotwaliwa maeneo yao wamekua wasikivu kipindi chote cha uhakiki wa ardhi hadi kufikia siku ya malipo kijijini hapo.

"Vilevile napenda kuipongeza TRC kwa kuweza kushirikiana na na sisi wataalamu wa Ardhi ili kazi ifanyike kwa uhakika na ufasaha zaidi na pia nawapongeza kwa kuweza kulipa fidia kwa wananchi na hii inaonesha zoezi lipo makini na mradi wa reli ya kisasa unaendelea vizuri" ameongeza Bwana Elias Gunze.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Isabilo Bwana Peter Masolwa amesema anaishukuru TRC kwa kuweza kulipa fidia kwa wananchi wake waliotwaliwa ardhi kwani itarahisisha kwao kununua mashamba mengine na viwanja waweze kujenga mahali pengine.

"Asilimia kubwa wananchi wangu ni wakulima na hizi fedha walizopata wataenda kununua mashamba waweze kuendelea na kilimo pamoja na ufugaji" alisema Masolwa.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Isabilo Bw. Kamuli Balugwa amesema eneo lake lilitwaliwa kwaajili ya kupisha ujenzi wa reli ya kisasa kuelekea Mwanza, ameipongeza TRC kwa kuweza kufika kijijini hapo na kuwalipa fidia watu wote waliotwaliwa ardhi.