TRC YAFANYA USAFI UWANJA WA NDEGE DODOMA.

June
2025
Shirika la Reli Tanzania - TRC limeungana na Taasisi zingine kutoka Wizara ya Uchukuzi kufanya usafi katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma ikiwa ni sehemu yamaadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma pembezoni mwa ukumbi wa Mikutano wa Jakaya kikwete kuanzia 01 -06 Juni, 2025.
Zoezi hilo la usafi wa kiwanja cha ndege unadhihirisha ushirikiano mkubwa wa kiutendaji uliopo baina ya taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi katika kutunza na kulinda mazingira kuboresha ustawi na maendeleo ya nchi.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Mratibu wa kitengo cha jamii na Mazingira TRC Dk. Veronica Milambo amesema kuwa Shirika la Reli Tanzania limechukua hatua madhubuti inayoendana na kauli mbiu ya Kitaifa ya maadhimisho ya Wiki ya mazingira duniani inayosema "Mazingira yetu na Tanzania ijayo Tuwajibike sasa: Dhibiti Matumizi ya Plastiki"
Kwa kudhibiti matumizi ya plastiki na taka nyinginezo kwa kuhakikisha ina vifaa madhubuti vya kuhifadhi taka ndani na nje ya majengo ya stesheni na ndani ya treni na maeneo yote ya ofisi za TRC pia hatua mbalimbali zimezingatiwa katika kutupa taka na kuzifanyia urejeshaji ili kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za usafirishaji.
Katika hatua nyingine Taasisi hizo Juni 04, 2025 zinatarajiwa kutembelea Stesheni Kuu ya Samia Suluhu (SGR) Dodoma, na kupanda miti kama sehemu ya kuenzi Maadhimisho hayo.