TRC YAENDELEA NA ZOEZI LA UTOAJI ELIMU NA UHAMASISHAJI KWA UMMA KUPISHA MRADI WA UJENZI WA SGR MWANZA - ISAKA

October
2021
Shirika la Reli Tanzania linaendelea na zoezi la utoaji elimu, kuhamasisha umma na uhamishaji wa makaburi ili kupisha ujenzi wa Reli ya Kisasa katika vvijiji sita (6) vya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu, hivi karibuni Oktoba 2021.
Katika zoezi hilo la utoaji elimu, uhamasishaji na uhamishaji wa makaburi kwa wananchi wa maeneo ambayo zoezi Hilo limefanyika, ndugu wa marehemu wameendelea kushirikiana na timu inayosimamia zoezi hilo wakiwemo maafisa Afya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, maafisa kutoka Shirika la Reli Tanzania _TRC pamoja na watendaji wa wa vijiji husika ili kuhakikisha zoezi linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Elimu hii ni endelevu kwa kipindi chote ambacho mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa ukiendelea katika maeneo mbalimbali.TRC inaendelea kuwashukuru watanzania kwa kuendelea kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh.Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendelea kuimarisha sekta ya miundimbinu ya Reli nchini.
Shirika la Reli Tanzania linawaahidi wananchi endapo TRC itatwaa Ardhi,makazi ya wananchi inawahakikishia kuwalipa stahiki kwa haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao kama kilimo kwa kuwa wengi wamejitambulisha ni wakulima na wanahitaji fedha kujiandaa kwani msimu wa mvua unakaribia kuanza ili waandae mashamba tayari kwa shughuli za kilimo.
Bwana Joseph Masanja ni miongoni wa mwanachi katika kijiji cha Gulung’wash ameeleza takribani makaburi 143 yameshahamishwa na anaishukuru serikali imeboresha zoezi la ufukuaji tofauti na mwanzo kwani hivi sasa ndugu wa marehemu wanapewa fursa ya kushiriki katika zoezi zima la kuhamisha na kuzika na hata kufanya tamaduni na mila kabla ya kuzika.
katika zoezi hilo zaidi ya vijana takribani sitini (60)kwa siku upata kibarua cha kufukua na kuchimba makaburi kitu ambacho wengi wao wamesema licha ya kuwa kazi ngumu lakini imewanufaisha kiuchumi kwani kwa siku Wana uhakika wa kupata fedha ya kujikimu na kufanya shuguli nyingine za maendeleo.