Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YAENDELEA NA ZOEZI LA FIDIA KUPISHA MRADI WA SGR MWANZA NA SHINYANGA


news title here
18
June
2022

Shirika la Reli Tanzania – TRC limeendelea na zoezi la malipo ya fidia kwa wanachi waliotwaliwa maeneo yao kupisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa mkoani Shinyanga na Mwanza, hivi karibuni Juni 2022.

Malipo ya fidia yanaendelea kwa lengo la kutwaa ardhi kwaajili ya kukabidhi eneo kwa mkandarasi wa mradi wa SGR kipande cha tano Mwanza – Isaka chenye urefu wa KM 361.

Zoezi limefanyika katika vijiji vya Lugembe, Sumbigu na Bukigi mkoani Shinyanga na vijiji vya Mwagala na Nyamatala Misungwi mkoani Mwanza ambapo takribani hundi 302 zimekabidhiwa kwa wahusika.

Mwenyekiti wa kijiji cha Sumbigu bwana Simon Masunga amezungumzia kuhusu mradi wa SGR kwa kusema kuwa “Zoezi tumelipokea, mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa nao unaendela hakuna malalmiko yoyote na zoezi la fidia limefanikiwa katika kijiji changu”

Baadhi ya wananchi waliopokea fidia zao wamefurahishwa na hatua ya Serikali ya kulipa fidia kwa wakati. Pia wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu, watumishi wa Serikali na benki kwa kukamilisha zoezi la fidia katika maeneo hayo.

Aidha, mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa Mwanza – Isaka umefikia 6.83% kazi kubwa zikiwa ni ujenzi wa tuta, vivuko, makalavati na madaraja. Kasi ya ujenzi inaenda sambamba na upatikanaji wa ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali imefanikisha kukabidhi eneo kwa mkandarasi kuendelea na ujenzi.