Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YAENDELEA NA KAMPENI YA UELEWA KUHUSU MAJARIBIO YA MIFUMO YA UMEME KATIKA RELI YA KISASA


news title here
17
May
2022

Timu ya mawasiliano kutoka Shirika la Reli Tanzania – TRC limeendelea na kampeni ya uelewa kuhusu majaribio ya mifumo ya umeme katika reli ya kisasa mkoani Morogoro Mei 17, 2022.

TRC inaendelea na kampeni ya uelewa yenye lengo la kutoa elimu kwa makundi tofauti katika jamii zinazoishi karibu na miundombinu ya reli kisasa. Kupitia kampeni ya uelewa maafisa wa TRC wanaendelea kuitahadharisha jamii hatua za kuchukua wanapokuwa karibu na reli ya kisasa pamoja na mambo ya kufanya ili kuhakikisha wanakuwa salama.

Majaribio ya mifumo ya umeme katika reli ya kisasa yalianza kufanyika Aprili 17, 2022 yakiambatana na kampeni ya uelewa mkoani Dar es Salaam na Pwani kupitia mikutano ya wananChi, shuleni, matangazo na vyombo vya habari.

Aidha kampeni ya uelewa tayari imefanyika katika maeneo ya Ngerengere, Mikese, Mtego wa Simba na Mkambalani pamoja na Shule zilizo maeneo hayo mkoani Morogoro. Ruben Chabaliko, Mwenyekiti wa kijiji cha Mkambalani ameeleza namna wananchi walivyoipokea elimu hiyo katika vitongoji vya kijiji cha Mkambalani

“Nashukuru sana Shirika la Reli wamekuja leo kutoa elimu wameanzia kitongoji cha Mbuyuni, wananchi wamepata elimu kubwa ya ujio wa reli ya mwendokasi, ni vizuri wakazingatia elimu iliyotolewa kwamba ni umeme mkubwa wananchi wameipokea vizui, wameelewa na wamezingatia elimua ya kutumia vivuko rasmi”

Mtaalamu wa Masuala ya Kijamii Kampuni ya Yapi Merkezi kipande cha Ngerengere – Morogoro Bi. Martha Makenge ameeleza hatua iliyofikiwa katika zoezi la utoaji elimu huku akisisitiza kuwa wananchi wamepewa tahadhari zaidi kuhusu maeneo ya kuvuka

“TRC na Yapi Merkezi tunaendelea na zoezi la kutoa elimu kuhusu masuala ya umeme, tumeanzia Dar es Salaam (KM 0) na tutaendelea hadi eneo la mwisho (KM 201), tumekuwa tukitoa tahadhari kwa maeneo yasiyo rasmi ambayo wananchi walikuwa wakipita lakini pia tumefungua rasmi vivuko vya juu na vya chini ili wananchi watumie katika kipindi hiki ambacho tunaendelea na majaribio”