Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

ZIJUE FAIDA ZA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA – SGR KIPINDI CHA UJENZI NA MARA BAADA YA UJENZI KUKAMILIKA


news title here
14
May
2019

Kupitia sera ya kitaifa na mkakati wa nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni Dhahiri na lazima kwa taifa kuwa na miundombinu imara. Ujenzi wa reli ni nguzo kubwa katika kuchochea na kupunguza gharama na muda wa safari kwa abiria na mizigo. Mataifa yenye nguvu duniani yamejengwa na kujikita katika kuwa na miundombinu imara kwenye utoaji wa huduma za usafiri wa haraka kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo ni mlango wa nchi zingine katika kupitisha bidhaa kwenda na kutoka, hii ni fursa kubwa kwa taifa kuwekeza kwenye miundombinu imara ya usafirishaji kwa wakati, salama na kwa bei nafuu. Wataalamu wa mambo ya usafirishaji duniani wanasema usafiri wa reli hupunguza gharama ya bidhaa kwa asilimia kati 30% hadi 40% na huwa ni kichocheo kikubwa cha uchumi.

Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa SGR ni Dares Salaam – Mwanza na itaunganisha mikoa ya Daressalaam, Pwani, Morogoro, Dodoma (makaomakuu), Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Nchi za maziwa makuu kama Uganda, Rwanda, Kongo na Burundi. Pia usanifu wa awali na upembuzi wa kina waujenzi wa Tabora–Kigoma, kaliua – Mpanda– karema ili kuunganisha na ziwa Tanganyika pamoja na nchi za kongo, Burundi na Rwanda unaendelea na ujenzi wake.

TRC imekwishakamilisha usanifu wa ujenzi wa reli kutoka Tanga –Kilimanjaro–Arusha- musoma na itaungnishwa na reli ya kati kupitia shinyanga na kutengeneza mtandao wa reli kwa mikoa ya kasikazini kupitia bandari ya Tanga Kwa upende wa kusini, TRC imekwishakamilisha usanifu wa ujenzi wa reli ya kusini kwa kuinganisha bandari ya Mtwara na mikoa ya Mtwara, Ruvuma na nchi za jirani Malawi na Zambia na kuitumia bandari ya Mtwara

FAIDA ZA UJENZI WA RELI YA KISASA KIPINDI CHA UJENZI

Mradi wa SGR Mradi mpaka sasa umetoa Fursa za ajira kwa jamii zipatazo 8,265 za moja kwa moja na mradi huu umechangia kukuza vipato vya wananchi ambao wanashiriki katika ujenzi wa SGR.

Mradi wa SGR umechangia katika pato la taifa na sera ya viwanda kufanya vizuri zaidi kwa maana mradi umeongeza mahitaji makubwa ya saruji na nondo pamoja na vifaa vingine vya ujenzi hivyo kuvifanya viwanda vya ndani kupata soko la bidhaa zake.

Mathalani kwa kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro kiasi cha nondo kilo milioni 45 za kiwango cha BS 500 kinachozalishwa hapa nchini kinatumika na saruji mifuko trakribani million 3 na kwa kipande cha Morogoro Makutupora ni Kilo milioni 70, na saruji mifuko milioni 6.4 huu ni mchango mkubwa sana katika mtandao kutoka viwandani kwenda kwenye mradi ukihusisha wadau mbalimbali kwenye ununuzi na usafirishaji ambapo itahitaji mzunguko takribani 16,000 wa saruji.

Mradi wa SGR umezalisha kazi kupitia mfumo wa mtandai (Supplying chain) ambapo Wafanyabiashara katika Sekta ya usafirishaji wamefaidika na mradi wa SGR, baadhi ya watanzania wamekodisha magari yao pamoja na kushiriki moja kwa moja katika usafirishaji wa vifaa na mitambo mbalimbali, hali hii imechochea ukuaji wa kipato kwa wananchi wa Tanzania.

Wakandarasi wazawa wamepata fursa ya kushiriki moja kwa moja kutoa huduma ambapo jumla ya wazabuni wapatao 500 wanashiriki na kati yao 15 ni kandarasi za kati kwenye ujenzi wa SGR na kujifunza ujuzi ambao haukuepo mwanzoni katika Sekta ya ujenzi nchini.

FAIDA ZA MRADI WA SGR KIPINDI CHA UENDESHAJI WA RELI YA KISASA

Kuongeza soko la ndani na kuimarisha Shilingi ya Tanzania (economy localization) hii ni kutokana treni kutumia umeme utakaozalishwa nchini, kama tungetumia mafuta diesel ambayo ni lazima kuagiza ingeongeza gharama kubwa kwa uendeshaji na matumizi ya akiba ya fedha za nje na Matumizi ya umeme inapunguza garama mara tatu endapo ingetumika mafuta na hali hii itasaidia kupunguza gharama kwa Nchi.

Treni za kisasa zitaweza kupunguza mrundikano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam kwa kuhakikisha mizigo inayowasili bandarini kusafirishwa kwa haraka na kuingizia mapato Nchi.

Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa Malori 500 barabarani ya mizigo.

Reli ya Kisasa itapunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya magari makubwa kwenye barabara na kupelekea kupunguza ajali na kufanya barabara kuwa njia salama zaidi ya usafiri.

Uokoaji muda wa kusafiri kwa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani maeneo ambapo reli hiyo itapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, DRC na Kenya.

Kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara na pesa hizo Serikali itaweza kuboresha huduma za kijamii kwa kutumia pesa ambazo zingetakiwa kufanya matengenezo ya barabara ambazo zingeharibika kutokana na mzigo mkubwa.

Kuongeza ufanisi wa utendaji na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa kupunguza muda wa safari mathalani Dar es salaam – Morogoro safari kuwa Saa1 na Dakika 15, safari ya DSM – DODOMA kutumia muda wa Saa 3 na treni itakua na uwezo wa kwendea mara 8 kwa siku Dodoma.

Kupunguza gharama za usafirishaji mizigo kwa wafanyabiashara inategemewa mara mradi utakapoanza gharama za usafirishaji wa mizigo itashuka kwa asilimia 40% na kuifanya bandari ya Dar es salaam kuwa na ushindani.

Kuchochea uanzishwaji wa viwanda katika maeneo mengine ya nchi, mradi utatoa uhakika wa usafirishaji wa malighafi na bidhaa na kuipatia fursa nchi kwenye uwekezaji wa miradi kwani ukiondoa Daresalaam na Pwani maeneo mengine ya nchi gharama za ardhi zipo chini.

SGR inachochea uanzishwaji wa miji midogo: sehemu zinazojengwa stesheni huwa zinaongeza chachu ya uanzishwaji wa makazi ya watu kutokana kuwa na uhakika wa usafiri. Maeneo ya Soga, Ruvu na Kwala kwa Mkoawa Pwani yatumike kupanga makazi ya watu na itaiongezea reli faida ya abiria na mizigo.

Kwa kuhitimisha usanifu na ujenzi wa reli hii umezingatia mazingira ya Tanzania hivo basi gharama za safari zitazingatia mazingira ya nchi na si kwa gharama za sehemu au bara linguine kama ulaya kwani treni za nchi hizo huzingatia usafirishaji wa abiria na mizigo mikubwa ambayo wanaweza safirisha kwa reli na kwa gharama za safari ya abiria ni nafuu.