Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YAENDELEA KUTOA FURSA YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANANCHI WA MPWAPWA MKOANI DODOMA


news title here
13
March
2021

Shirika la Reli Tanzania - TRC linaendelea kutoa fursa ya mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi waliotwaliwa na ardhi na kupisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa - SGR kipande cha pili Morogoro - Makutupora , yaliyo fanyika katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Machi 2021 hivi karibuni.

TRC imeendeleza mafunzo hayo ya ujasiriamali katika maeneo mbalimbali ikiwemo kijiji cha Godegode na Kimagai mkoani humo ambapo wananchi walipata fursa ya kujifunza kupitia wakufunzi katika fani tofauti.

Wakufunzi hao ni pamoja na Afisa ardhi na maliasili, Afisa kilimo na mifugo, Afisa maendeleo ya jamii pamoja na fundi nguo, watengenezaji batiki na wajasiriamali mbalimbali.

Afisa maendeleo ya jamii kutoka wilaya ya Mpwapwa Bw. Baraka Msuya amewaasa wananchi kuwa na uthubutu na kuchangamkia fursa mbalimbali ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kujiingizia kipato kwa lengo la kuleta maendeleo katika jamii zao.

“Uthubutu na kujitoa ndio ngao kubwa ya kufanikiwa na kuleta maendeleo katika jamii zetu“ alisema Bw. Msuya.

Aidha Bw. Msuya alisema kuwa wananchi lazima wajijengee tabia ya utunzaji wa fedha pindi wanapoanzisha biashara na pia kuwa wabunifu wa kuangalia fursa kulingana na wakati .

Naye Mkazi wa kijiji cha Godegode wilayani humo Bw. Ramadhan Boke amefurahishwa sana na mafunzo hayo ya ujasiriamali nakusema kuwa yataleta mwanga kwa wanakijiji kwa kupata kujifunza mambo mbalimbali bila ya gharama yeyote.

“Wanakijiji tumepata fursa kama hii, sio ya kuichezea kwani italeta matokeo chanya" alisema Bw. Boke.