Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​TRC YAANZA KUTOA HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA KATI YA DAR ES SALAAM NA MOSHI


news title here
07
December
2019

Shirika la Reli Tanzania - TRC laanza kutoa huduma ya usafiri wa treni za abiria iliyokuwa imesimama kwa zaidi ya miaka 25 kati ya Dar es Salaam na Moshi, safari hiyo imeanza rasmi katika stesheni ya Kamata jijini Dar es Salaam hivi karibjni Desemba, 2019.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini - LATRA Mhandisi Dkt. John Ndunguru ameshuhudia kuanza kwa huduma hiyo mara baada ya kujiridhisha kufuatia majaribio ya treni kupita katika reli ya kaskazini hivi karibuni Desemba 01, 2019 kuanzia Dar es Salaam hadi Moshi mkoani Kilimanjaro.

Aidha, wananchi wameonesha kuipokea huduma ya usafri wa treni Dar - Moshi kwa furaha ambapo Shirika kwa sasa litakuwa likifanya safari ya treni ya kisasa ya Deluxe mara mbili kwa wiki katika siku za Ijumaa na Jumanne kutoka Dar es Salaam na Jumamosi na Jumatano kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt. John Ndunguru amewaomba abiria wote ambao wanaosafiri na treni ya Deluxe kuwa mabalozi wazuri kuitangaza treni hiyo, pia amewataka wananchi kuendelea kutunza na kulinda miundombinu ya reli kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Focus Sahani amewashukuru wananchi walioamua kusafiri na treni ya Deluxe kwa kuwa wanaunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kurejesha huduma za usafiri katika maeneo ambayo huduma hizo zilisitishwa kwa muda mrefu.