TRC YAENDELEA NA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA
February
2019
Shirika la Reli Tanzania laendelea kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam ambao maeneo yao yamepitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR awamu ya kwanza Dar es Salaam – Morogoro katika mitaa ya Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Mtaa wa Sabasaba na Miembe Madafu katika kata ya Ukonga hivi karibuni Februari 2019. Zoezi la fidia kwa mkoa wa Dar es Salaam laendelea katika Mitaa ya Gulu Kwalala katika kata ya
Gongo la Mboto, Mtaa wa Miembe Madafu pamoja na Mtaa wa Sabasaba katika wilaya ya Ilala mkoani, wananchi zaidi ya 600 wanatarajiwa kulipwa fidia katika mitaa hiyo ili kupisha Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kisasa – SGR. Zoezi ni endelevu kwa wananchi wote ambao maeneo yao yamepitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kuanzia Dar es Salaam hadi mkoani Dodoma. Shirika la Reli Tanzania linawasisitiza wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kutoa
ushirikiano kwa maafisa wa TRC wakati wa zoezi la ulipaji fidia kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anayestahili kulipwa fidia analipwa ili kukabidhi eneo kwa Mkandarasi na kumuwezesha kumaliza Mradi ndani ya muda uliopangwa.